Profesa Matthew Luhanga afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Matthew Luhanga amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Mawasiliano na Habari wa UDSM, Dkt. Dotto Kuhenga amethibitisha kutokea kwa kifo hicho Septemba 16,mwaka huu wakati akipatiwa matibabu.

“Ni kweli tumempoteza Profesa Luhanga ambaye alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo chetu kwa muda mrefu. Siwezi kuzungumzia zaidi kuhusu ugonjwa wake, lakini alikuwa amelazwa hospitali,” amesema Dkt. Kuhenga.

Dkt.Kuhenga ameeleza wasifu wa Profesa Luhanga akisema aliajiriwa rasmi katika chuo hicho kama mhadhiri mwaka 1978 baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka miwili kama mhadhiri wa muda wakati huo akiwa ofisa elimu.

Amesema, mwaka 1982, alipandishwa cheo na kuwa mhadhiri mwandamizi.

Pia mwaka 1986, alipanda na kuwa profesa mshiriki na mwaka 1990 akawa profesa kamili, akiwa ni mmoja kati ya maprofesa wachache nchini waliofikia hatua hiyo.Jifunze kuhusu yeye chini ya makala fupi ya video hapa chini.
Amesema, mbali na kuwa kiongozi wa chuo, Profesa Luhanga amekuwa mjumbe wa bodi mbalimbali na ameandika machapisho mengi hasa katika sekta aliyobobea ya mawasiliano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news