Serikali yatenga trilioni 2.03/- kuzikwamua kaya maskini nchini

Na James K. Mwanamyoto,Dodoma

Serikali imetenga kiasi cha shilingi trilioni 2.03 kwa ajili ya kuzikwamua kaya zote maskini nchini kutoka katika lindi la umaskini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF kilichoanza 2020 mpaka 2023.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akitoa neno la utangulizi wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa semina ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.

Mhe. Mchengerwa amesema, kwa kuwa Serikali imetenga fedha za kutosha kuzifikia kaya zote maskini, amewaomba wajumbe wa kamati hiyo kufanya ufuatiliaji ili kaya zote maskini zinazostahili kupata ruzuku zinanufaika.

“Kama kuna kaya yoyote maskini imesahaulika, nawaomba mtupatie taarifa haraka ili watendaji wetu wazifikie na kukamilisha taratibu za kuwawezesha kupata ruzuku na kuongeza kuwa, katika utekelezaji wa awamu hii, Serikali itahakikisha kila Mtanzania anayestahili kunufaika na mpango huu, anapata ruzuku,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa alipokuwa akitoa neno la utangulizi wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema licha ya TASAF kuziwezesha kaya maskini kiuchumi, pia imewawezesha watoto wa kike wanaotoka kwenye kaya hizo maskini kupata elimu kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Humphrey Polepole (Mb) ameipongeza Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa azma yake ya kutenga fedha za kutosha kuziwezesha kaya zote maskini nchini.

Mhe. Polepole amesema, azma ya Mhe. Samia ya kutenga fedha hizo inaonesha nia ya dhati ya Serikali yake na Watendaji wake ya kuzikwamua kaya zote maskini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Humphrey Polepole (Mb) akizungumza wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Baadhi ya Watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakimsilikiza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Humphrey Polepole (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya TASAF iliyofanyika kwenye Ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Bw. Ladislaus Mwamanga akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyofanyika kwenye Ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.


Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wakisikiliza mada kuhusiana na utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyowasilishwa kwao na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani).

Akiwasilisha mada kwa kamati hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga amesema, idadi ya kaya za walengwa katika utekelezaji wa Mpango wa TASAF, Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu inatarajiwa kufikia milioni moja laki nne na nusu, hivyo wanufaika kwenye kaya hizo watakuwa zaidi ya watu milioni 10.

Bw. Mwamanga amesema, ofisi yake imetekeleza zoezi la utambuzi wa kaya maskini kwa kushirikisha jamii na viongozi katika maeneo husika ili kutatua changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa awamu iliyopita.

Katika kuhakikisha hakuna udanganyifu wakati wa zoezi la uandikishaji wa kaya maskini, Watendaji wanaohusika na zoezi hilo wamesainishwa kiapo cha kutekeleza jukumu hilo kwa uadilifu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news