Tanzania kuwa mwenyeji onesho la Utalii Jumuiya ya Afrika Mashariki

Na Happiness Shayo-WMU

Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Tanzania itakuwa mwenyeji wa kwanza wa onesho la Utalii wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EARTE).

Lengo la onesho hilo hapa nchini ni kuvutia na kukuza uwekezaji katika sekta ya Utalii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma , Mhe. Masanja amesema onesho hilo litakuwa linafanyika kwa mzunguko katika nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kila mwaka.

"Onesho la EARTE litafanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 9 hadi 16 Oktoba, 2021 ambapo litajumuisha siku tatu za maonesho na siku tano za ziara maalum ya kutembelea vivutio vya utalii pamoja na fursa za utalii wa ndani kwa Tanzania Bara na Zanzibar," amesema Mhe. Masanja.

Wakati huo huo amefafanua kuwa, kwa kutambua Utalii kama sekta mtambuka onesho hilo ni fursa muhimu ya kuhamasisha uhifadhi wa Maliasili na Malikale.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akitoa rai kwa watanzania hususan wakazi wa Arusha kuhamasika na Onesho la Utalii la Jumuiya ya Afrika Mashariki mapema leo Jijini Dodoma. Wakwanza Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga na Wapili kutoka ni Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT), Dkt, Abdulla Juma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news