MWENYEKITI wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam, Nassoro Idrissa Mohamed amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).
Nassoro ametangazwa kutwaa nafasi hiyo Novemba 29,2025 katika Uchaguzi Mkuu wa TPLB jijini Dar es Salaam, baada ya kumuangusha mpinzani wake Hosea Lugano kwa kupata kura 7 dhidi ya 6, ambapo kura moja iliharibika.
Wapiga kura kwenye uchaguzi ni timu 16 za Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini mbili hazikushiriki mkutano huo.Hosea ni Mwenyekiti wa klabu ya Namungo ya Lindi na pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Lindi, ambapo pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
Hata hivyo juzi alijiuzulu Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, ili pate fursa ya kuwania uenyekiti wa bodi baada ya kuelezwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuwa kuendelea kwake na mchakato wa uchaguzi , huku akiwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kulikuwa na mgongano wa kimaslahi.
Mwenyekiti huyo mpya wa TPLB alikuwa Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo, lakini tangu Juni mwaka huu alikuwa akikaimu nafasi ya Mwenyekiti baada ya kujiuzulu kwa Steven Mnguto.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo








