Thierry Hitimana atangazwa kocha msaidizi Simba SC

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wamemtangaza Kocha Thierry Hitimana (42) raia wa Rwanda kuwa kocha wao msaidizi kwa lengo la kuimarisha kikosi chao.
Taarifa hizo zinakuja muda mfupi baada ya kuripotiwa kuwa Kocha wao Mkuu raia wa Ufaransa, Didier Gomes hatoruhusiwa kukaa katika benchi katika michuano ya kimataifa kama hatokuwa na CAF License A au UEFA Pro License ambayo hana.

Inaonekana Hitimana ambaye ana CAF License A ndiye atashika mikoba wakati huu unaodaiwa kuwa Gomes atakuwa anapambana na kozi.

Thiery alitua siku mbili nchini akitokea kwao Rwanda, ambapo safari yake ilikuwa ni kurudi Mtibwa Sugar aliyokuwa amewahi kuitumikia katikati ya msimu kisha kung'atuka kwa madai ya kutoelewana na wasaidizi wake kwenye benchi la ufundi.

Post a Comment

0 Comments