Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Zacharia HansPope afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Uongozi wa Klabu ya Simba umeeleza kupokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Zacharia HansPope ambaye amefariki dunia usiku huu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa fupi iliyotolewa na Uongozi wa Klabu hiyo leo Septemba 10,2021.

UVIKO-19 inaua!!!!


HANS POPPE NI NANI?

Kama anavyotambulishwa, jina lake ni Zacharia Hans Poppe, ambaye alizaliwa mwaka 1956 mjini Dar es Salaam na kukulia mkoani Iringa.

Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, Zacharia alijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambako alifikia cheo cha Kapteni, kabla ya kuachishwa kazi na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, kwa tuhuma za uhaini, dhidi ya Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka 1983.

Lakini mwaka 1995, Zacharia aliachiwa huru kwa msamaha wa Rais wa Awamu ya Pili, Alhaj Ally Hassan Mwinyi, mwezi mmoja kabla hajamuachia Ikulu ya Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu.

Kama zinavyosema sheria za nchi, mtu aliyehukumiwa kifungo, hana haki ya kugombea wadhifa wowote au kuajiriwa tena, Zacharia naye hakuweza kurejea kazini, badala yake akaamua kujiajiri, kwa kuanzisha miradi yake mwenyewe, ambayo  ikiwa ni miaka kadhaa sasa, miradi hiyo imesimama imara.

HANS POPE NA SIMBA SC:

Alianza kuipenda Simba SC mwanzoni kabisa mwa miaka ya 1970, akiwa kijana mdogo na zaidi mwenyewe anasema, mechi ambayo ilimfanya ajitamke rasmi yeye ni Simba damu ilikuwa dhidi ya wapinzani wa jadi, Yanga Juni 23, mwaka 1973, ambayo Wekundu wa Msimbazi, walishinda 1-0, bao pekee la Haidari Abeid ‘Muchacho’ dakika ya 68.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news