Wanaodhaniwa kula chakula chenye sumu waruhusiwa kurudi nyumbani

Na Dotto Mwaibale, Singida

WATU 50 waliokuwa wamelazwa Hospitali ya Mkoa wa Singida wakipatiwa matibabu baada ya kunusurika kufa baada ya kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu wameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya afya zao kuimarika.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Binilith Mahenge akimjulia hali, Mwanahamisi Shabani ambaye ni mjamzito mmoja wa wananchi ambaye amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Singida akipatiwa matibabu akidhaniwa kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Binilith Mahenge alipowatembelea wananchi hao Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Banuba Deogratius amesema walipokea jumla ya wagonjwa 50, wanawake 34 na wanaume 16 ambapo hali hadi leo hali zao zilikuwa zikiendelea vizuri na baadhi yao wameanza kuwaruhusu kurudi nyumbani kuendelea na majukumu yao ya ujenzi wa Taifa.

Banuba amesema, wakazi hao wa Kata ya Unyambwa Kijiji cha Kisasida katika Manispaa ya Singida mkoani hapa walifikishwa hospitalini hapo baada ya hali zao kuwa mbaya kutokana na kula chakula kilichoandaliwa katika shughuli za ufunguzi wa Madrasa moja katika kijiji hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Binilith Mahenge akimjulia hali na kuzungumza na Sheikh wa Kata ya Unyambwa, Ramadhani Yusuf (kulia) ambaye amelazwa katika hospitali hiyo akipatiwa matibabu akidhaniwa kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu. Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi,ASP Stella Mutabihirwa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Binilith Mahenge akiwajulia hali wahanga wa tukio hilo alipowatembelea kabla ya kuruhusiwa.

Akipokea taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Bilinith Mahenge amewapongeza madaktari wa hospitali hiyo kwa jitihada walizozifanya za kuhakikisha wananusuru maisha ya wananchi hao ambapo kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri na kuipongeza Serikali kwa kuweka miundombinu mizuri ya huduma katika sekta ya afya.

Ametoa wito kwa viongozi wa Serikali na dini kuwajibika kikamilifu katika kutoa elimu ya namna ya kuandaa chakula pamoja na kusimamia inapotokea sherehe mbalimbali kwenye maeneo yao ili kuepuka madhara ya namna hiyo yasije kutokea tena.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi, ASP Stella Mutabihirwa amesema wanawashikilia watu saba kuhusika na tukio hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Binilith Mahenge akiwajulia hali wahanga wa tukio hilo alipo watembelea kabla ya kuruhusiwa.
Wahanga wa tukio hilo wakiwa hospitalini hapo kabla ya kuruhusiwa.
Wahanga wa tukio hilo wakiwa hospitalini hapo kabla ya kuruhusiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi, ASP Stella Mutabihirwa, akizungumza na madaktari wa hospitali wakati mkuu wa mkoa alipowatembelea wahanga wa tukio hilo.

Amesema, katika tukio hilo mtoto mmoja mwenye umri wa miaka saba aliyemtaja kwa jina la Fahad Masoud alifariki dunia kabla ya kufikishwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news