Waziri Mkuu amsimamisha kazi Afisa Manunuzi wilayani Karagwe

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Afisa Manunuzi wa Wilaya ya Karagwe Bw. Yesse Kaganda baada ya kutoridhishwa na viwango vya ubora wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karagwe ambayo imejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.5.
Waziri Mkuu amesema Rais Mheshimiwa Samia ametoa pesa za kujenga na kukamilisha miradi ya maendeleo na kuhakikisha Serikali inasogeza huduma zote muhimu za kijamii lakini watendaji wachache wamekuwa wakishindwa kufuata maadili ya kazi zao na kujenga miradi isiyokuwa na ubora.

Ameyasema hayo leo Septemba 19, 2021 baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi mkoani Kagera.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi wa Mikoa na Wilaya wahakikishe wanasimamia vyema matumizi ya fedha zilizotolewana Rais Mheshimiwa Samia katika kutekeleza miradi ya maendeleo na huduma za jamii ili kuleta tija na mabadiliko kwa wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua marumaru zilizowekwa kwenye Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya wilaya ya Karagwe na baada ya kutorishishwa na ubora wake aliamuru ziondolewe na ziwekwe nyingine zenye viwango vinavyofanana na pesa iliyotolewa na Serikali. Alikuwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera Septemba 19, 2021.

“Malengo ya Rais wetu sasa yanaenda kutimia kwani anataka kila mwananchi apate huduma za afya hukohuko aliko, kuanzia ngazi ya kijiji tunajenga zahanati na baada ya kuwa zahanati za kutosha tunajenga kituo cha afya ambacho kina huduma zote muhimu, kama upimaji wa magonjwa yote, chumba cha upasuaji, jengo la mama na mtoto pamoja na wodi za wanaume na wanawake”. Alisema

Waziri Mkuu amewahakikishia wakazi wa Wilaya ya Karagwe kuwa ujenzi wa Hospitali hiyo utakamilika kwa wakati na kwa viwango kwani tayari fedha za kununua vifaa tiba vyote na mitambo ya mionzi zimetengwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Karagwe akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kagera, Septemba 19, 2021. Kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI (Elimu), David Silinde.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Hospitali ya Wilaya ya Karagwe, Septemba 19, 2021. Kulia ni Naibu Waziri TAMISEMI (Elimu), David Silinde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

“Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kila wakati anasisitiza usimamizi mzuri wa fedha zinazotolewa ili zitumike kwa ukamilifu na kujenga miradi yenye ubora, vigae hivi havijaanza kutumika tayari vimechakaa, Afisa Manunuzi huyu akae pembeni kwanza na vigae vipya viwekwe kwa gharama zake.”

Amesema wananchi pia wana wajibu wa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kutoa maoni kwani miradi hiyo inatekelezwa kwa kodi za wananchi. “Ninawaomba wananchi muendelee kuwa na imani na Serikali yenu pamoja na viongozi wake

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news