Amuua ndugu yake kwa kukataa kuchangia 1500/- ya nyama waliyokula mjini Moshi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Ndungi katika Wilaya ya Moshi kwa tuhuma za kumuua ndugu yake, William Shoo kwa madai ya kukataa kuchangia nyama ya sh.1, 500 waliyonunua.
Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 11, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema mauaji hayo yalitokea Oktoba 10, 2021 asubuhi baada ya marehemu kugoma kuchangia nyama hiyo waliyonunua.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, kabla ya mauaji hayo mtuhumiwa alinunua nyama kwa kushirikiana na marehemu ambapo walikula pamoja na walipomaliza kula alikataa kuchangia chochote ndipo ugomvi ukaanza.

Amesema, katika ugomvi huo, mtuhumiwa alimkata ndugu yake na kitu chenye ncha kali kichwani na kusababisha kifo chake.

"Awali kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa alinunua nyama kwa kushirikiana na mwenzake, ambayo ina thamani ya Sh1, 500 walipokula pamoja ndugu yake huyo alikataa kulipia, ndipo ugomvi ukaanza ambapo ilipelekea kuchukua maamuzi hayo ya kumkata na kitu chenye ncha kali,"amesema.

Wakati huo huo, jeshi hilo linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumuua John Nyaki kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake, wakimtuhumu kuiba mizani.

Kamanda Maigwa, amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 6, 2021, asubuhi katika eneo la Kibosho Dakau Wilaya ya Moshi mkoani hapa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news