Bernard Membe apewa mbinu za kisheria kwenda kuchukua fedha zake Bilioni 6/- kutoka kwa Cyprian Musiba

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe ameshauriwa namna ya kuweza kulipwa fedha zake kiasi cha sh.Bilioni 6 na mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba kama ilivyoamuliwa katika hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kumuweka ndani mdaiwa.

Ushauri huo imetolewa na Flugence Massawe ambaye ni Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha LHRC nchini.

"Mshinda tuzo mheshimiwa Bernard Membe ana nafasi ya kufanya utekelezaji wa hukumu chini ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Madai.

"Kwa mfano anaweza kuomba kukamata mali zake au hata akaunti ya benki au kumuweka ndani kama mfungwa wa madai ,muombaji anaweza kuomba kumpelekea ndani kwa gharama zake ,unamgharamia anafungwa gerezani, lakini anapofungwa haimaanishi deni linaisha anaweza akatoka na bado ukaendelea kumdai na unaweza kuomba kumrudisha tena ndani,"amesema.
Hivi karibuni, Cyprian Musiba aliamuriwa kumlipa Mheshimiwa Bernard Membe kiasi hicho cha fedha kama fidia ya kumchafua kupitia vyombo vyake vya habari.

Hukumu hiyo ni ya shauri la kesi namba 220 ya mwaka 2018 ambayo ilitolewa na Jaji Joacquine De Mello ambapo amesema mbali na mambo mengine Musiba amlipe sh.Bilioni 6 Membe, pia inatoa zuio la kudumu la kutomkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake na kulipa gharama za kesi.

Mahakama imesema sh.Bilioni 5 ni fidia ya hasara halisi na sh. Bilioni 1 hasara ya jumla.

Katika kesi hiyo Membe alimshtaki Musiba, Mhariri wa gazeti la Tanzanite na wachapishaji wa gazeti hilo ambapo aliwadai sh. Bilioni 10 kwa kumchafua.

Musiba katika kesi hiyo alishtakiwa kwa kumtuhumu Membe kuwa anamhujumu Rais John Magufuli asitekeleze majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo huku akidai kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo ni maandalizi anayofanya kugombea urais mwaka 2020 kupitia CCM.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news