Bodi ya Ushauri TARURA yaridhishwa na ujenzi madaraja yanayotumia mawe

Na Erick Mwanakulya, Kigoma

Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeonesha kuridhishwa na ujenzi wa madaraja yanayojengwa kwa kutumia Teknolojia ya mawe mkoani Kigoma.
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TARURA wakipita kwenye daraja la mawe Kurugongo linalounganisha vijiji vya Kurugongo na Titye lenye urefu wa mita 22.4 likiwa limefikia asilimia 80 kukamilika katika ziara ya ukaguzi wa miradi Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, Kulia ni daraja la miti linalotumika na wakazi wa vijiji hivyo.

Madaraja hayo yanajengwa kwa kutumia nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Mfadhili wa Mradi wa Kilimo Endelevu katika Mkoa wa Kigoma (Sakrip – Enabel) na ujenzi wake unasimamiwa TARURA.

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TARURA wameonesha kuridhishwa na ujenzi wa madaraja hayo kwa kutumia Teknolojia ya mawe walipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi mkoani kigoma.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TARURA, Bi. Julieth S. Magambo alisema katika ziara ya siku tatu katika Mkoa wa Kigoma wameridhishwa na ujenzi wa madaraja hayo kwa kutumia teknolojia ya mawe kwa sababu ya unafuu wake kulinganisha na madaraja ya aina nyingine na kujiridhisha kuwa ujenzi huu unaokoa fedha nyingi.

“Tumeridhishwa sana na ujenzi wa madaraja haya kwa sababu gharama zake ni nafuu kulinganisha na madaraja yanayotumia zege pia yanachukua muda mchache kukamilika, yanachukua kuanzia wiki tatu hadi miezi mitatu kwa wananchi kuanza kutumia na kurahisisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi”, alisema Bi.Julieth.
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TARURA wakitazama sehemu ambapo ujenzi wa mfereji mkubwa utajengwa hili kupunguza adha ya mafuriko katika ziara ya ukaguzi wa miradi Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma.

Muyama yenye urefu wa Km 35 kiwango cha lami unaotarajiwa kluanza hivi karibuni kwa Mhandisi Baraka Mkuya katika ziara ya ukagzui wa miradi Halmashauri ya Wilaya Buhigwe, mkoani Kigoma.

Aidha, Bi. Julieth alisema faida ya kutumia teknolojia hiyo ni wananchi wenyewe kuilinda miundombinu ambayo wamejitolea katika ujenzi kwa ushirikishwaji wake wa kukusanya mawe, pamoja na wananchi husika kupewa mafunzo ya ujenzi wa madaraja hivyo kusaidia kuongeza ujuzi kwa wananchi.

Ameongeza kuwa, changamoto kubwa ni kipindi cha kilimo kwa sababu mwananchi anatakiwa ajitolee kwenye ujenzi na ashiriki kwenye kilimo.

Pia, Bi. Julieth alisema ni vyema kuendelea kuwekeza katika teknolojia hii ya ujenzi wa madaraja ya mawe katika Mikoa mingine kwa sababu wamejiridhisha unafuu wake na kuomba ushirikiano katika maeneo mengine kwa wananchi kama walivyojitolea wananchi wa Kigoma.

Naye, Meneja wa TARURA Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Godwin Mpenzile ameishukuru Bodi ya Ushauri ya TARURA kwa kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa madaraja ya mawe na kuridhishwa na ujenzi wa madaraja hayo.
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TARURA wakipata maelezo ya ujenzi wa barabara ya Kasulu – Kabanga – Mwanga – Kasumo –
Mhandisi Mpenzile alisema kuwa madaraja ya mawe Mkoani Kigoma yamesaidia sana kuondoa changamoto za vivuko. Vilevile aliongeza kuwa TARURA Mkoa wa Kigoma ipo katika mpango wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa Km 35 kwa kiwango cha lami inayokatiza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, pamoja na ujenzi wa mfereji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.

“TARURA Mkoa wa Kigoma tumeanza usanifu wa barabara ya Kasulu – Kabanga – Mwanga – Kasumo – Muyama yenye urefu wa Km 35 kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake utaanza hivi karibuni, pia ujenzi wa mfereji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ili kuondoa adha ya mafuriko kwa wananchi wa Wilaya hiyo”, alisema Mhandisi Mpenzile.

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TARURA wamefanya ziara ya siku tatu ya ukaguzi wa miradi ya madaraja ya mawe katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Buhigwe, Uvinza na Kigoma na kuridhishwa na ujenzi wa madaraja hayo pamoja na gharama zake na kutoa wito kuwa teknolojia hiyo isambae katika maeneo mengine.

Post a Comment

0 Comments