CCM yatetea Jimbo la Ushetu kwa asilimia 96 ya kura, wabakiza nne

NA MWANDISHI MAALUM

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ushetu Mkoa wa Shinyanga, Bw. Linno Mwageni amemtangaza Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Emmanuel Peter Cherehani kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 9, 2021 Cherehani alipata kura 103,357  sawa na asilimia 96.6 dhidi ya mshindani wake, Bw. Mabula Nkwabi Julius wa ACT Wazalendo aliyepata kura 3,588 sawa na asilimia 3.4.

Uchaguzi huo umefanyika kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Elias John Kwandikwa ambaye pia alikuwa Waziri wa Ulinzi kufariki Agosti 2, 2021.Zinazohusiana, ACT WAZALENDO washinda ubunge Jimbo la Konde.

Kwa mujibu wa taarifa, katika jimbo hilo idadi ya wapiga kura walioandikishwa walikuwa 165,418.

Aidha,  idadi ya waliopiga kura ilikuwa 107,188 huku halali zikiwa 106,945 na kura zilizokataliwa zilikuwa 243.

Post a Comment

0 Comments