Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria yapokea taarifa ya utekelezaji wa Sheria ya Ajira kwa Wageni nchini

NA MWANDISHI MAALUM

SERIKALI imesema kufuatia uwepo wa sheria za wageni nchini na wawekezaji kumesaidia kuwepo mfumo wa uratibu na mamlaka ya kusimamia shughuli za sekta hiyo ili kuleta ustawi wa watanzania na Taifa kwa ujumla.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa sheria ya ajira kwa wageni katika ukumbi wa Bunge, Oktoba 26, 2021 Jijini Dodoma.

Hayo yalisemwa Oktoba 26, 2021 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ilipokutana na kupokea taarifa ya utekelezaji wa sheria ya ajira kwa wageni nchini katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.

Waziri Mhagama amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inasimamia Sheria za Kazi na miongoni mwa sheria hizo ni Sheria ya kuratibu ajira za wageni Na 1. ya mwaka 2015 ambapo sheria hiyo imeweka masharti kwa wageni wanaokuja kufanya kazi nchini.

“Uwepo wa Sheria ya kuratibu ajira za wageni nchini Na. 1 ya mwaka 2015 ilipelekea kuanzishwa kwa mamlaka ya utoaji wa vibali vya ajira kwa wageni, hivyo kwa kuzingatia matakwa ya sheria hii wawekezaji na waajiri wanaokusudia kuajiri wageni nchini wanapaswa kuwasilisha maombi kwa Kamishna wa Kazi na hati maalum ya kibali cha ajira itatolewa kwa mgeni husika,” alisema Waziri Mhagama.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia kikao cha kamati hiyo katika Ukumbi wa Bunge, Oktoba 26, 2021 Jijini Dodoma.

Mheshimiwa Mhagama aliongeza kuwa kutokana na uwezekaji mzuri unaoendelea nchini, Serikali imewataka wawekezaji ama makampuni yaliyoajiri wageni kuweka utaratibu wa urithishaji wa ujuzi kwa wazawa ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao pindi wageni hao wanapokuwa wamemaliza muda wao wa kufanya kazi nchini.

Naye Naibu waziri Ofisi ya waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi alisema kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa kuomba vibali kielektroniki kulikuwa na mlolongo mrefu hali iliyosababisha uwepo wa vishoka na viashiria vya rushwa hivyo uombaji kupitia mfumo huo wa vibali vya kielekroniki kutavutia wawekezaji zaidi.

Akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa sheria ya ajira kwa wageni mbele ya kamati hiyo Kamishina wa Kazi Brig. Gen. Francis Mbindi amesema Mfumo wa kushughulikia vibali vya kazi kwa njia ya kieletroniki umeongeza makusanyo ya maduhuli ya serikali.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika ukumbi wa Bunge, Oktoba 26, 2021 Jijini Dodoma.
Kamishina wa Kazi Brig.Gen. Francis Mbindi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa sheria ya ajira kwa wageni mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Ukumbi wa Bunge, Oktoba 26, 2021 Jijini Dodoma.

“Jumla ya bilioni 17 zimekusanywa kama ada ya vibali vya kazi kuanzia Mwezi Januari hadi kufikia Mwezi Seoptemba mwaka huu ikilinganishwa na kiasi cha billioni tatu zilizokusanywa kuanzia Mwezi Julai hadi Septemba 2020 kupitia mfumo wa zamani wa kushughulikia vibali vya kazi,” alibainisha Brig.Gen. Mbindi.

Naye Mjumbe wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na sheria Mhe. Edward Ole Lekaita amepongeza mabadiliko yaliyofanywa na serikali ambayo yameleta matokeo chanya na kuendela kulinda ajira za wazawa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news