Madiwani watoa Azimio kumpongeza Rais Samia kwa kuwapa Bilioni 2.93/-

NA MOHAMED HAMAD

Madiwani wa Halamashauri ya Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, wametoa Azimio la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa Shilingi Bilioni 2.93 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wananchi.
Akisoma Azimio hilo, Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mheshimiwa Edward Olekaita, alisema Wilaya ya Kiteto imepata fedha nyingi zinazotokana na UVIKO-19 ambazo zimeelekezwe kwenye miradi ya wananchi ambayo awali kulikuwa na changamoto kubwa.
Alitaja fedha hizo kuwa ni Bilioni 1.14 za ujenzi wa madarasa 57 za shule shikizi 14, mradi wa vituo viwili vya Afya wa thamani ya Milioni 500 vitakavyojengwa Tarafa ya Olboloti na Kujungu, ununuzi wa gari la Afya.

Zingine ni Milioni 400 kwa ajili ya mradi wa maji Kata ya Kaloleni, ununuzi wa mashine ya kisasa ya X-ray Digital ambayo itaondoa adha kwa wananchi kufuata huduma Hospitali za mikoa ya Jirani Dodoma na Arusha, ujenzi wa nyumba moja ya walimu watakaoishi wawili ya mil 90 na ujenzi wa madarasa 44 shule za Sekondari.

“Tunamshukuru sana sana, Mama Samia Suluhu Hassan,  Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutupatia fedha hizi zitapunguza changamoto za maendeleo zinazokabili wananchi, vijana wa siku hizi wanasema Mama ameupiga mwingi,"alisema Mbunge Ole Lekaita.

Alisema, fedha za UVIKO-19 zimekuwa na tija Kiteto hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mbaraka Al Haji Batenga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kiteto, John John Nchimbi, Wakuu wa Idara za Halmashauri, Waheshimiwa Madiwani na wananchi wote wanamshukuru sana Mhheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha hizo ambazo zitatumiwa kwa uadilifu katika miradi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Abdallah Bundalah, alisema fedha hizo zitasimamiwa kikamilifu na kuagiza madiwani wilayani humo kuhakikisha wanasimamia kwa ukaribu miradi ya maendeleo ya wananchi akisema baada ya muda wataonyesha umma namna walivyotumika fedha hizo katika miradi ya wananchi.

Nao baadhi ya madiwani akiwemo Hassan Benzi wa Kata ya Dosidosi, Rehema Cheleleu viti maalumu Tarafa ya Olboloti na Paulo Tunyoni wa Kata ya Partimbo, walieleza kuwa wananchi walikuwa na changamoto za kutopata huduma za jamii kwa wakati hivyo fedha hizo zitapunguza adha iliyowakabili wananchi kwa muda mrefu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news