Rais Samia ateua viongozi mbalimbali, atengua uteuzi wa RC Shinyanga

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:-
1. Amemteua Mhe. Sofia Edward Mjema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mhe. Mjema anachukua nafasi ya Dkt. Philemon Sengati, ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Mjema alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

2. Amemteua Mhe. Jaji Omar Othman Makungu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Makungu alikuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar.


3. Amemteua Mhe. Jaji Mustapha Siyani kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo Jaji Siyani alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Eliezer Felishi aliyeteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Uteuzi huu umeanza tarehe 07 Oktoba, 2021. Wateule hao wataapishwa tarehe 11 Oktoba, 2021 saa 05:00 Asubuhi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 8, 2021 na Jaffar Haniu ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news