Ratiba ya Kombe la Shirikisho barani Afrika

NA MWANDISHI MAALUM

Simba SC watamenyana na Red Arrows ya Zambia katika mchujo wa kuwania Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho wakianzia nyumbani Novemba 28,2021 kabla kwenda Lusaka kwa mechi ya marudiano Desemba 5.

Katika droo iliyofanyika mchana wa leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Jijini Cairo, Misri ikiongozwa na gwiji wa Misri na klabu ya Zamalek, Ismail Youssef na Mkuu wa Idara ya Mashindano ya CAF, Khaled Nassar, suala la Biashara United na Ahli Tripoli ya Libya bado linatafutiwa suluhisho.

Biashara United ilishindwa kutokea uwanjani Jijini Benghazi Jumamosi nchini Libya kumenyana na wenyeji, Al Ahly Tripoli katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili kwa matatizo ya usafiri.

Mwenyekiti wa Biashara United, Suleiman Mataso alisema kwamba ndege waliyoomba kusafiri nayo awali iliahirisha safari hiyvo wakalazimika kukodi ndege ya shirika la Tanzania (ATCL), lakini wakakosa vibali vya kutua kwenye nchi ambazo wangepitia kabla ya kutua Benghazi.

Alisema baada ya hapo Biashara waliomba msaada Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwaombea CAF mechi yao isogezwe mbele hadi Jumanne ili wapate vibali vya anga vya kutua kwenye nchi watakazopitia.

Hata hivyo taratibu zote za mchezo zilifuatwa Uwanja wa Martyrs of February jijini Benghazi Jumamosi baada ya wenyeji Al Ahli kufika na baada ya muda wa kikanuni, waamuzi wakamaliza mchezo kwa tafsiri Biahsara United haikutokea uwanjani.

Hata hivyo,jana usiku huo TFF ilitoa taarifa kwamba bado wanasubiri majibu kutoka CAF kuhusu ombi la kusogezwa mbele mchezo huo.

Ikumbukwe mechi ya kwanza Biashara United inayofundishwa na kocha Mkenya, Patrick Odhiambo anayesaidiwa na mzawa, Marwa Chamberi ilishinda 2-0 Oktoba 15, mabao ya Deogratius Judika Mafie dakika ya 40 na Atupele Green Jackson dakika ya 61.
Aidha, timu zilizofuzu ni Zanaco (Zambia) – Binga (Mali), Simba (Tanzania) – Red Arrows (Zambia), TP MAzembe (DR Congo) – MarumoGallants (South Africa).

ASEC Mimosas (Cote d’Ivoire) – GD Interclube (Angola), Nouadhibou (Mauritania) – Coton Sport (Cameroon)
US Gendarmerie Nationale (Niger) – DC Motema Pembe (DR Congo).

AS Otoho (Congo) – Gor Mahia (Kenya),
APR (Rwanda) – RS Berkane (Morocco),
Tusker (Kenya) – CS Sfaxien (Tunisia),
Hearts if Oak (Ghana) – JS Saoura (Algeria),
Rivers United (Nigeria) – Al Masry (Egypt),
Stade Malien (Mali) – Ahly Tripoli (Libya) au Biashara United (Tanzania).

Al Ittihad (Libya) – Enyimba (Nigeria),
AS Maniema Union (DR Congo) – Pyramids (Egypt),LPRC Oilers (Liberia) – Orlando Pirates (South Africa), Royal Leopards (Eswatini) – JS Kabylie(Algeria).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news