SERIKALI YATENGA BILIONI 2.2/- KUNUNUA MBEGU ZA ALIZETI

Na Doreen Aloyce,Dodoma

ILI kupunguza uhaba wa mafuta nchini na kuinua Sekta ya Kilimo cha Alizeti, Serikali imetenga shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya kuandaa mbegu bora za alizeti.
Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Waziri wa Kilimo, Profesa Aldof Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema, walipanga kupata tani 5,000, lakini wamefanikiwa kupata tani 1,600 za mbegu hizo.

Aidha amesema hii ni mara ya kwanza Serikali imetekeleza suala la mbegu,hivyo kila mmoja lazima apate mbegu hizo kwa sababu ni bei rahisi.

"Mbegu hizi zitakuwa zinapatikana katika halmashauri na kwa bei rahisi ili kuokoa fedha zinazotumika kwa ajili ya kununua mafuta, "amesema Profesa Mkenda.

Amesema,Serikali imejipanga kuhakikisha mwakani hawaagizi tena mbegu nchini Ufaransa,wanahitaji kuona mbegu bora zinapatikana hapa nchini.

Amesema,Serikali imekuwa ikitumia Shilingi nusu Trilioni kila mwaka kwa ajili ya kuagiza mafuta jambo ambalo halikubaliki kabisa, wanahitaji kuona mafuta yawe yanapatikana hapa nchini.

Amefafanua zaidi kuwa wameteua mikoa mitatu ambayo italima alizeti chini ya usimamizi mzuri ili yaweze kuzalisha mbegu za alizeti mikoa hiyo na wilaya zake wamegawana ekari kwa ajili ya kulima zao hilo katika mikoa hiyo.

Profesa Mkenda amegawa mbegu kwa Wakuu wa Wilaya ambapo zitapelekwa katika halmashauri kwa ajili ya kwenda kuwauzia wananchi ambao ni wakulima.

Mbali na hilo amesema, wameongeza fedha za mafunzo kwa maafisa ugani na mabwana shamba ili waweze kuwapa maelekezo mazuri wakulima.

Mbali na hilo amesema watazidi kuyapa kipaumbele mazao ya Pamba, Michikichi, Karanga na mengine ili kumaliza uhaba wa mafuta nchini.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa Dkt.Fatma Mganga alisema wemetenga ekari 800,000 kwa mkoa wa Dodoma ambapo kila wilaya itapata ekari zake kwa ajili ya kupanda mbegu hizo.

Amesema tayari wilaya zimeshapewa ekari za kulima ambapo mbegu hizo zitapatikana katika halmashauri mbalimbali hapa jijini Dodoma.

Hata hivyo, amempongeza Waziri Profesa Mkenda kwa kazi nzuri anayoifanya kwa ajili ya kuinua Kilimo cha alizeti hapa nchini.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Bahi ambae alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dodoma Antony Mtaka,Mwanahamisi Mkunda alimuhakikishia Waziri wa Kilimo kuwa mbegu hizo zitatumzwa vizuri na wakulima wote watazipata

Alisema kilio cha wakulima wa Alizeti kitazidi kukua hapa nchini.

Naye Mkulima Stephen Marriale kwa niaba ya wakulima wenzake ameishukuru serikali kwa hiki walichokifanya na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujali sekta ya Kilimo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news