Waziri Profesa Ndalichako atoa maagizo matano kuhusu Bilioni 64.9/-

Na Doreen Aloyce,Diramakini Blog

WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametoa maelekezo matano katika utekelezaji wa kiasi cha Shilingi Bilioni 64.9 kilichopokelewa na wizara hiyo kutoka kwenye fedha za UVIKO-19 ikiwemo kuhakikisha miradi yote iliyopangwa inakamilika kabla au ifikapo Mei 30,mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dodoma, Profesa Ndalichako ametaja maeneo mengine kuwa ni kuimarisha elimu ya mafunzo na ufundi stadi na kuimarisha mazingira ya elimu ya ualimu na kuongeza idadi ya walimu.

Amesema katika maeneo hayo matatu wataongeza uwiano wa vitabu Ili kusaidia wanafunzi wenye uoni hafifu na wasioona ,kununua vifaa saidizi,kujenga mabweni katika chuo cha ualimu Morogoro.

Ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati Profesa Ndalichako amesema,  ni lazima maandalizi yote yanayohusu fedha hizo yakamilike ifikapo Oktoba 30,mwaka huu lakini pia matokeo ya utekelezaji wa mradi yaendane na thamani ya fedha zilizotengwa,na vifaa vyote vinunuliwe kwa bei ya soko.

Aidha,amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo aandae mfumo mahsusi wa uratibu,ufuatiliaji na utekelezaji wa mradi ili kubaini changamoto na kuzitafutia ufumbuzi na kutolewa taarifa za utekelezaji kila mwezi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news