Wanawake wazidi kupaisha soka la Tanzania, CECAFA Challenge Women’s 20 waanza kwa ushindi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Clara Luvanga dakika ya 90 ameongeza furaha kwa Watanzania baada ya kuiwezesha timu ya Tanzania kusonga mbele.
Ni kupitia michuano ya wasichana chini ya umri wa miaka 20 Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge Women’s 20) baada ya kuichapa Eritrea 1-0 jioni ya leo Uwanja wa FTC Njeru nchini Uganda.

Kwa ushindi huo, timu hiyo itashuka tena dimbani Jumatatu kumenyana na Burudani kabla ya kuivaa Ethiopia Jumatano, Uganda Jumamosi ijayo na kukamilisha mechi zake kwa kucheza na Djibouti Novemba 9, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments