Waziri Prof.Mkenda:Mbegu ya alizeti itauzwa 3500/- kwa kilo moja

NA MWANDISHI MAALUM

Waziri wa Kilimo, Mhe.Prof. Adolf Mkenda amezindua rasmi zoezi la mpango wa usambazaji wa mbegu za alizeti kwa wakulima, huku akiagiza mbegu hizo kuuzwa kwa kilo moja sh. 3,500 kwa wakulima.Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda akimkabidhi mfuko wa mbegu ya alizeti zilizozalishwa na Wakala wa Mbegu za Kilimo(ASA), Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga wakati wa uzinduzi wa Mpango wa usambazaji wa mbegu za Alizeti nchini.

Akizungumza na wakulima, pamoja na wadau wa zao la alizeti katika ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo,Kilimo4 mkoani Dodoma, Waziri Mkenda amesema, Serikali imeweka mkakati kuhakikisha changamoto ya mbegu inakwisha kwa miaka michache ijayo.

Amesema, kwa mara ya kwanza serikali imetenga zaidi ya sh.bilioni 2.2 kwa ajili ya kuzalisha mbegu bora za alizeti karibu tani 2,000.

Waziri amewataka wafanyabiashara kuwekeza katika kilimo cha alizeti hasa katika uzalishaji wa mbegu ili waweze kupata fedha kwa haraka kutokana na uwepo wa soko la uhakika.
Waziri wa Kilimo,Prof. Adolf Mkenda akiteta jambo na Dkt. Sophia Kashenge Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo(ASA)katikati, Kulia ni Mkuu wa Kitengo wa Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Kilimo Bw. Hudson Kamoga.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkundi.

Ameongeza kuwa, mahitaji ya mbegu za alizeti ni makubwa hapa nchini ambapo kwa sasa zimepatikana tani 1,600 hadi 2000 huku mahitaji halisi yakiwa ni tani 5,000.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dkt. Sophia Kashenge amesema,kama taasisi inaendelea kufuata maelekezo ya Wizara ya Kilimo na kuhakikisha changamoto ya mbegu inakwisha.

Amesema, mbegu hizo zitauzwa kwa shilingi 3,500 kwa kilo moja kama Waziri wa Kilimo alivyoagiza huku akiwataka wakulima kununua mbegu hizo kwa bei nafuu kutoka kwa Wakala wa Serikali.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatuma Mganga amesema, kama mkoa wamejipanga kuhakikisha mbegu hiyo ya alizeti inawafikia wakulima kupitia halmashauri zao kwa bei iliyoelekezwa na serikali.
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda akimkabidhi Mwenyekiti wa wakulima wa Alizeti Bw. Steven Maleale mfuko wa mbegu ya alizeti zilizozalishwa na Wakala wa Mbegu za Kilimo(ASA), wakati wa uzinduzi wa Mpango wa usambazaji wa mbegu za Alizeti nchini.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatma Mganga(Kulia) na Mwenyekiti wa wakulima wa alizeti Bw. Steven Maleale baada ya kukabidhiwa mifuko ya mbegu na Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda kama ishara ya uzinduzi wa usambazaji wa mbegu ya alizeti nchini

Amesema, kupitia wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri hizo ufanisi wa kilimo cha alizeti katika maeneo yao ndio itakuwa kipimo chao cha kazi na kuongeza kuwa, hategemei kama wilaya ama halmashauri mojawapo itashindwa kufikia malengo.

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Mwanahamisi Munkunda ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi,amesema, maelekezo yote ya serikali yaliyotolewa juu ya mbegu za alizeti kwa wakulima yatafanyiwa kazi kulingana na umuhimu wake nakuongeza kuwa mkoa wa Dodoma kama miongoni mwa mikoa ya kimkakati utafanya vizuri katika kilimo cha alizeti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news