NA LUSUNGU HELELA-WMU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza leo Jijini Arusha kwenye mkutano baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi ya Sekta binafsi Tanzania ( TPSF) uliolenga kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazokabili sekta ya utalii nchini hususani katika kipindi cha UVIKO-19 ambapo aMEfafanua itakavyozitumia fedha ya kiasi cha shilingi bilioni 90.2 walizopewa kutoka kwenye fungu la fedha za mapambano ya UVIKO-19 ya shilingi trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF).
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania ( TPSF), Angelina Ngalula akizungumza leo jijini Arusha kwenye mkutano baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi ya Sekta binafsi Tanzania ( TPSF) ameihakikishia Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya utalii nchini.Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro leo Jijini Arusha wakati wa mkutano wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Sekta Binafsi ( TPSF) uliolenga kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazokabili sekta ya utalii nchini hususani katika kipindi cha UVIKO-19.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya utalii nchini wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wakati wa mkutano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPS) uliolenga kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya utalii nchini ambapo amesema fedha iliyotolewa na Shirika la Fedha Duniani itasaidia kunyanyua sekta ya utalii nchini kwa kuimarisha miundombinu.Amefafanua kuwa, vifaa vitakavyonunuliwa kwa ajili ya vifaa vya kupimia UVIKO 19 vitasambazwa maeneo yote ya vivutio vya utalii ili kuwasaidia watalii pindi watakapopimwa wapewe majibu yao huko huko tofauti na ilivyo sasa.
”Tumedhamiria kuondoa usumbufu ili watalii watakapokuja nchini wasiweze kupata usumbufu kwa kuhakikisha kila hifadhi inaweza kutoa huduma hizo kwa haraka ili kuwafanya watalii wasikae kusubiri matokeo kwa muda mrefu,”amesisitiza Dkt.Ndumbaro.
Mwenyekiti wa Chama cha Wasafrishaji Watalii Tanzania (TATO), Willy Chambulo akizungumza wakati wa mkutano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPS) uliolenga kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya utalii nchini ambapo amempongeza Waziri Ndumbaro kwa kazi nzuri anayoifanya katika Wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akizungumza leo jijini Arusha kwenye mkutano baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi ya Sekta binafsi Tanzania( TPSF) ameihakikishia Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea kushirikiana na katika kutatu changamoto zinazoikabili sekta ya utalii nchini.”Barabara ikiwa nzuri na wewe una hoteli yako ipo ndani sana Watalii watakuja kulala katika hoteli yako kwa sababu kuna barabara nzuri, hivyo hela hii inakwenda kufanya kazi hiyo,”amesema Dkt.Ndumbaro.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi ( TPSF), Angelina Ngalula amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kujitoa kuisaidia sekta ya Utalii nchini.
”Tunaomba salamu zifike kwa Mhe. Rais kwa juhudi za kuendeleza utalii kwa kututafutia fedha kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF).Tumemuona anavyoipambania sekta ya utalii kupitia kipindi chake maarufu alichokiasisi cha Royal Tour ambacho kimeongeza ujasiri kwa Wawekezaji wa sekta ya utalii nchini, tunampongeza sana Rais wetu,”amesema Mwenyekiti wa TPSF, Ngalula.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt.Allan Kijazi (kulia) pamoja Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania ( TPSF), Angelina Ngalula wakiwasikiliza viongozi wa wadau wa utalii wakitoa maoni ya namna ya kuboresha sekta ya utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Wadau wa utalii mara baada ya mkutano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPS) uliolenga kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya utalii nchini Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania ( TPSF) Angelina Ngalula na kulia Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi