Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo yashinda nafasi ya pili Drafti SHIMIWI 2021

NA ELEUTERI MANGI

Mchezo wa Drafti kwa wanawake umemalizika ambapo katika fainali hiyo iliyozikutanisha timu za Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo iliwakilishwa na mchezaji Niuka Chande na timu ya Ofisi ya RAS Morogoro ambayo iliwakilishwa na Leokadia Mwango’ombe ambaye ndiye bingwa wa mchezo huo .
Nafasi ya pili katika mchezo huo imeenda kwa Niuka Chande wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo huku nafasi ya tatu ikienda kwa Neema Makasi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) kwenye Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) 2021 yanayofanyika Manispaa ya Morogoro.

Ushindi huo wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambao umechezwa leo Oktoba 31, 2021 mjini Morogoro umeanzia katika makundi manne yaliyokuwa na wachezaji wanne kila kundi huku yeye akipangwa katika kundi D ambalo alianza mbio za kuusaka ushindi kwa kuwafunga wapinzani wake na kuibuka kinara katika kundi hilo.

Akizungumzia ushindi huo, Niuka amemshukuru Mungu kwa kumjalia afya njema hatua iliyomsaidia kufanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano hayo ambayo yalikuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na kila timu kusaka ushindi na kuziwakilisha timu zao vema.
“Kweli viongozi wetu wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha timu yetu ya Wizara inafanya vizuri. Naushukuru wetu kwa kuwa imara na kusimamia timu zetu vizuri,” amesema Niuka.

Kwa upande wa wanaume Wizara hiyo iliwakilishwa na Omari Mataka ambaye naye alishika nafasi ya tatu katika kundi lake.

Mchezo huo unaongozwa na kanuni ambazo ndiyo zimekuwa nguzo ya ubingwa wa mchezo huo ikiwemo muda wa mchezo utakuwa sio zaidi ya dakika 30, michezo unachezwa mara mbili kama ni lazima itakuwa mitatu, kufikiri ni dakika moja ikizidi utanyang’anywa ushindi (utapoteza mchezo), ukigusa kete unawajibika kucheza hakuna kuacha/kurudisha na hakuna kugongewa/kumsaidia ikibainika aliyesaidiwa atanyang’anywa/atanyimwa ushindi (atapoteza mchezo).

Kanuni nyingine zinawataka watazamaji watakaa mita tatu kutoka kwenye mchezo, wachezaji watalazimika kuzima simu wakati wote wa michezo, mchezo kuwa na mwamuzi na mshindi atapata pointi 2 na sare pointi 1.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news