Anaswa akibaka nguruwe machinjioni

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKAZI wa Kijiji cha Mavanga kilichopo katika kata ya Mavanga wilayani Ludewa mkoani Njombe anayefahamika kwa jina la Afro Nyigu (31) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumbaka mnyama aina ya Nguruwe.
Ramadhani Kihanga ambaye ni Afisa Mtendaji wa kijiji hicho amesema kuwa, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 14, 2021 ambapo mtuhumiwa huyo alifika katika machinjio ya wanyama hao huku akiwa amelewa na kukuta nguruwe akiwa amefungwa kamba kwa maandalizi ya kuchinjwa ndipo kijana huyo alimvamia na kufanya nae mapenzi.

Amesema,wakati akiendelea na tendo hilo mlinzi wa machinjio hiyo alikuwa ametoka kidogo na aliporejea alimkuta kijana huyo akiendelea kufanya kitendo hicho ambapo alimkamata na kumpigia simu balozi na mtendaji wa kijiji ambao walifika katika eneo hilo la tukio.

Amesema kuwa, walipomuhoji kijana huyo sababu za kufanya kitendo hicho alidai ni maamuzi yake binafsi hivyo hapaswi kuulizwa ambapo viongozi hao wakamchukua na kumkabidhi mikononi mwa polisi.

“Kitendo alichokifanya huyu kijana mwenzetu ni cha kusikitisha sana! Tunaomba sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wengine maana kama ameweza kufanya hivi kwa mnyama anaweza kufanya uharibifu hata kwa binadamu,” amesema Kihanga.

Akizungumza kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Njombe, Hamiss Issa na mtandao huu amesema ni kweli tukio hilo lipo na kwa sasa Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wa tukio hilo na mtuhumiwa amehifadhiwa katika kituo cha Polisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news