Angola yainyeshea mvua ya magoli 12-0 Zanzibar michuano ya CANAF, Sierra Leone yaifumua Uganda 3-0

NA JOHN MAPEPELE

MABINGWA watetezi wa Mashindano ya Afrika kwa mchezo wa Mpira wa Miguu kwa wenye Ulemavu CANAF 2021 timu ya Angola leo, Novemba 28, 2021 wameonyesha kwamba wao ni mabingwa wa Dunia katika mchezo huu baada ya kuichabanga Zanzibar dazeni moja kwa nunge kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Angola (jezi nyekundu) wakikabiliana na wachezaji wa Zanzibar (jezi ya kijani mpauko) kwenye mchezo wa CANAF 2021 uliochezwa leo, Novemba 28,2021 jijini Dar es Salaam ambapo Angola imeshinda 12-0.

Katika kipindi chote Angola waliutawala mchezo huo kutokana na uzoefu mkubwa wa wachezaji wao wanaocheza katika mashindano ya kimataifa.

Kipindi cha kwanza tayali Angola ilikuwa inaongoza kwa magoli sita kwa nunge na katika kipindi cha pili wakaongeza magoli mengine sita na kufanikiwa kupata ushindi wa dazani moja kwa sifuri dhidi ya timu ya Zanzibar.

Magoli ya Angola yamefungwa na Kufula Hilario, Aharo Francisco, Joachim Sabino, Chiarere Jord na Pacincia Fblio.
Timu za Uganda (jezi nyekundu) na Timu ya Siera Leone (jezi nyeupe) wakiimba nyimbo zao za Taifa wakati wa mechi ya mashindano ya CANAF 2021 leo Novemba 28, 2021.

Wakati huo huo katika mchezo mwingine, Timu ya Siera Leone imeibamiza mabao 3- 0 ambapo bao la kwanza limefungwa katika dakika ya 15 na mshambuliaji Kuroma Ctbassy na goli la pili limefungwa dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza na goli la tatu dakika ya 43 kipindi cha pili na Lumeh Foday.

Mchezo huo ulitawaliwa na mvua kubwa hali iliyosababisha kushindwa kuendelea na kwa muda baada ya kipindi cha kwanza cha mchezo kumalizika kutokana na maji kujaa katika uwanja.

Mashindano haya yamezinduliwa rasmi jana Novemba 27 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa na yatakamilika Disemba 4, 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news