Chuo cha Maji, Mamlaka ya Maji Zanzibar waingia makubaliano

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Chuo cha Maji na Mamlaka ya Maji Zanzibar wameingia katika historia kubwa ya kukubaliana na kusaini Mkataba wa Makubaliano (Memorandum of Understanding) katika kuanzisha na kuendeleza mashirikiano katika masuala ya Mafunzo, Utafiti, Ushauri wa Kitaalam na Ubunifu.

Lengo ni kuhakikisha Mamlaka ya Maji Zanzibar inanufaika na uwepo wa Chuo cha Maji lakini pia Chuo kinafaidika na fursa zilizopo katika Mamlaka hiyo na kuhakikisha ile Zanzibar ya Blue inafikiwa kwa mafanikio ya haraka yatakayosaidia Taasisi hizi kufanya mabadiliko chanja kwa haraka zaidi.
Mkuu wa Chuo Dkt. Adam O. Karia na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Dkt. Salha Kassim wamesaini mkataba huo tayari kuanza kushirikiana mara moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news