Haji Manara aangua kilio uwanja wa ndege

NA MWANDISDHI DIRAMAKINI

MSEMAJI Mkuu wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amejikuta akibubujikwa na machozi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ( Julius Nyerere International Airport-JNIA) uliopo katika jijini Dar es Salaam baada ya kumuaga binti yake wa kwanza,Hamida kwenda masomoni nchini Uturuki.

Manara ni miongoni mwa watu mashuhuri zaidi nchini Tanzania hususani katika medali za soka huku akiwa mwenye ujasiri mkubwa katika kukisimamia kile ambacho anakiamini bila kuyumbishwa.
"Ilikuwa ni time (nyakati) ngumu zaidi kwangu wakati nikimsindikiza Airport Binti yangu Hamida aliyeongozana na Mama yangu,wakielekea Istanbul nchini Uturuki,ambapo mwanangu huyo wa kwanza anaenda kuanza masomo yake ya chuo kikuu.

"Ukiacha nyakati mnazokuwa safarini, maisha yangu yote nimeishi na Hamida wangu popote pale nilipoishi, sijui itakuwa vipi maisha bila mtu niliyeishi nae kwa miaka yake yote kumi na nane.

"Dada zangu mnaokuja nyumbani mara kwa mara, Zamaradi Mketema, Aunty Ezekiel, Hamisa Mobetto,Batuli (Yobnesh Yussuf Hassan),Monalisa (Yvonne Cherrie) na wengineo...
"Nimekuza, lakini nimeumia, nani atawahudumia juice na maji? Nani atawakaribisha nyumbani wageni wangu kwa smile (tabasamu) nzuri yenye bashasha na furaha? Hakika nimepigwa na chuma cha utosi, nimemzoea mno mwanangu huyu wa kwanza kwa sababu walau wengine for sometimes (wakati mwingine) wanakuwa boarding school (shule za bweni) au kwa Mama yangu, huyu nipo nae mwenyewe always (muda wote). Okay (sawa) kwangu ni kuendelea kumuombea dua ili aweze kufikia malengo yake InshaAllah.
"Nitakumiss my lovely daughter (nitakumisi binti yangu mpemdwa), na chozi langu la Airport (uwanja wa ndege) ni ishara ya kukutaka ukasome uje kurusha ndege kipenzi changu,"ameeleza Haji Manara.

Haji Manara na soka

Kabla ya kuwa, Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara alikuwa ni Msemaji wa Simba SC. Huyu ni mtoto wa Sunday Ramadhan Manara ambaye ni mzaliwa wa Kigoma, Mzee Sunday aliwahi kuwa mchezaji wa Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania.

Pia ni miongoni mwa wachezaji wachache waliowahi kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya Bara la Afrika ikiwemo Heracles ya Uholanzi (1976-78), New York Eagles (1978) na kutimkia Austalia katika klabu ya ya Australian (1980) na mwaka 1981 alienda kucheza soka Dubai katika Klabu ya Al Nasri iliyokuwa moja ya timu tishio katika Ligi Kuu ya Dubai na mwaka 1984 aliamua kurudi nyumbani na kustaafu rasmi kucheza soka.

Kwa msingi huo, Haji Manara licha ya kuwa maarufu kupitia soka, pia amekulia katika familia ya soka ambayo ilimpa mwanga na kumfikisha hapa alipo sasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news