Harmonize azama katika penzi nzito na mtoto mwingine wa Kizungu

NA GODFREY NNKO

RAJAB Abdul Kahali (Harmonize, Konde Boy au Teacher, Tembo na mengine mengi) ambaye ni miongoni mwa waimbaji staa na mtunzi wa muziki, mfanyabiashara kutoka nchini Tanzania ameingia katika uhusiano mpya na mrembo anayejulikana kwa jina la Briana.
Mrembo huyo ambaye anaonekana kupokelewa kwa mikono miwili na mashabiki, uraia wake unahusishwa na Italia pamoja na Australia.

Uhusiano huu unakuwa wa nne katika kipindi kifupi ukifuatiwa na ule wa karibuni na staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja ambaye waliachana katika mazingira ya kutatanisha ukiwemo wa mrembo kutoka Italia, Sarah na ule wa Jackline Wolper.

Harmonize ambaye alizaliwa Machi 15, 1990 katika Kijiji cha Chitoholi mkoani Mtwara ambapo alianza kuvuma na kibao cha Aiyola mwaka 2015, Bado, Matatizo (2016) na badaye akatoa wimbo na CEO wa Wasafi Classic Baby (WCB), Naseeb Abdul Juma Issack (Diamond Platnumz) kabla ya kuondoka katika lebo hiyo na kwenda kuanzisha ya kwake ambayo inaendelea kufanya vema.
Baada ya kuondoka mwaka 2019 aliamua kuanzisha lebo yake Konde Music Worldwide ambapo ndiye CEO hadi sasa, ambapo pia Septemba 7, 2019 alifunga ndoa na mpenzi wake raia wa Italia, Sarah Michelotti.

Ilikuwa ni siku chache baada ya mwanamuziki huyo kujiondoa rasmi katika kundi la Wasafi Classic Baby (WCB) ambalo linaongozwa na msanii maarufu Diamond Platinum.

Mwanamuziki huyo anayependa kujiita Konde boy akimaanisha kuwakilisha Wamakonde kutoka Kusini mwa Tanzania alimchumbia Sarah miezi michache na hakuwahi kutangaza siku rasmi ya harusi yake.

Harusi hiyo ambayo ilidaiwa kuwa ya siri ilifanyika siku ya Jumamosi na kuhudhuria na wageni 100 na hakuna msanii hata mmoja kutoka kundi lake la zamani la WCB aliyeudhuria tafrija hiyo maalum.

Aidha,2020, mwaka mmoja baada ya kubadilishana kwa viapo, ilitangazwa kuwa wenzi hao walikuwa wametengana kwa sababu ya tofauti zisizoweza kusuluhishwa ikiwemo kutuhumiana kuwa na uhusiano wa watu wa nje huku meseji zikinaswa walivyokuwa wanabadilishana taarifa na michepuko. Alikaa kwa muda mfupi, akaingia katika uhusiano na Farida Kajala ambao nao hawakudumu muda mrefu.
Hata hivyo, baada ya uhusianao kati ya Harmonize na Kajala kuvunjika ambapo ulionekana kuwa na mvuto wa kipekee huku wakichorana tatoo, ukimya ulitawala.

Baada ya kutawala ukimya, Novemba 16, 2021 Harmonize ametambulisha rasmi mrembo Briana anayejitambulisha kwa jina la @briana__tz huko Instagram kuwa ndiye mpenzi wake mpya.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Harmonize ameweka picha kadhaa za mrembo huyo ambaye inasemekana ni kutoka nchini Italia huku wengine wakisema ni kutoka Austarlia.

Harmonize amemtambulisha mrembo huyo kwa kuandika, "nilikuwa nikiusubiri wakati huu kwa muda mrefu sana ili niuthibitishe umma ni kiasi gani una maana kubwa kwenye maisha yangu".
Baada ya kumtambulisha mrembo Briana, Harmonize ameambatanisha na picha mbalimbali zikimuonyesha akiwa mjini Dallas nchini Marekani.
Harmonize akiwa amevalia fulana ambayo imebandikwa picha ya mpenzi wake mpya, Briana ambaye anajivunia kuwa ni sehemu ya faraja yake.
Picha ya mpenzi wa Harmonize, Briana kama ilivyotolewa rasmi na Harmonize katika ukurasa wake wa Instargram.

Post a Comment

0 Comments