Jiji la Dodoma laanza kuuza viwanja, Benki ya DCB kutoa mikopo ya kulipia

NA MWANDISHI MAALUM

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeanza kuuza viwanja katika eneo la Kikombo lililopo Mashariki mwa Jiji la Dodoma na Kusini mwa barabara ya kwenda Dar es salaam kwa umbali wa kilomita tatu.
Viwanja hivi vinauzwa ambapo kiwanja cha makazi ni shilingi 8000/m², makazi biashara shilingi 10,000/m², biashara shilingi 12,000/m², taasisi shilingi 8000/m², makazi maalum shilingi 8000/m² na viwanda vidogo shilingi 8000/m² kwa mfumo wa ushirikiano kati ya Jiji la Dodoma na Benki ya DCB ambapo mteja atakopeshwa.

Masharti

1. Mteja atatakiwa kufungua Akaunti katika Benki ya DCB

2. Mteja anatakiwa kulipa asilimia 10% ya gharama za kiwanja ambapo benki itampa mkopo wa asilimia 90% na kumkata kidogo kidogo kwenye mshahara ama biashara yake kila mwezi kulingana na makubaliano na thamani ya kiwanja.

3. Mkopo unaenda hadi miaka saba kwa kutegemea mapendekezo ya mteja


>Hata hivyo ikiwa Mteja atahitaji na mkopo wa kujenga nyumba DCB iko tayari hadi kumjengea nyumba

NB: Bei hii imeunganishwa na gharama za uwekaji huduma za kijamii ambazo ni maji, umeme na barabara za kiwango cha moramu.

Kwa mawasiliano piga namba 0659719184

Post a Comment

0 Comments