KMC FC yawabamiza Azam FC 2-1

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

KMC imepata ushindi wa kwanza wa msimu baada ya kuichapa Azam FC 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Ni katika mtanange wa aina yake ambao umepigwa katika dimba la Uhuru lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Waliopelekwa maumivu kwa Azam FC, ni Matheo Anthony Simon dakika ya 13 na Hassan Salum Kabunda dakika ya 90.

Aidha,la Azam FC walipata bao lao kupitia Charles Zullu dakika ya 43 ambapo kwa matokeo hayo, KMC inafikisha alama tano na kupanda kwa nafasi mbili kutoka mkiani katika ligi ya timu ya timu 16 ya Tanzania Bara.

Awali Kocha msaidizi wa KMC FC , Habibu Kondo amesema kuwa licha ya kuwa timu haina matokeo mazuri, lakini maandalizi yaliyofanyika katika kipindi hiki cha mapumziko yaliyokuwa yamepisha Timu ya Taifa yamefanikiwa kwa asilimia kubwa ikiwemo kurekebisha changamoto mbalimbali ambazo zilionekana katika michezo hiyo.

Habibu alifafanua kuwa hali ya kikosi ni nzuri ,ikiwemo morali za wachezaji ipo juu pamoja na fitness nzuri na kwamba licha kuwa mchezo wa huu utakuwa na ushindani mkubwa lakini kwa maandalizi ambayo yamefanyika yataleta matokeo mazuri.

Kondo aliongeza kuwa, mipango ya timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni ni kufanya vizuri katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kwamba licha ya kuwa na mwanzo ambao sio rafiki, lakini bado matumani makubwa ya kufanya vizuri yapo.

"Tunajua kuwa hatujaanza vizuri kwenye michezo yetu, lakini bado tupo kwenye ubora wetu, tumefanya maandalizi ambayo kimsingi yataleta matokeo chanya kikubwa mashabiki zetu wazidi kutupa ushirikiano,"alibainisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news