Kassim Dewji amrithi hayati Zacharia Hans Poppe uwenyekiti Simba SC

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah Muhene (Try Again) amemtangaza Kassim Dewji kuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo.

Salim amemtangaza Dewji wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2021 wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam (JICC) siku ya Novemba 21, 2021.

Dewji anachukua nafasi ya Zacharia Hans Poppe aliyefariki dunia mwezi Septemba, mwaka huu na kuzikwa kwao mkoani Iringa.

Katika mkutano mkuu wa klabu hiyo, Muhene amesema bodi imempendekeza Dewji kuchukua nafasi ya Poppe.“Tunafahamu uwezo Dewji, hivyo bodi imemkabidhi jukumu la kuongoza kamati ya usajili ambayo ilikuwa ikiongozwa na Poppe enzi za uhai wake. Ni mwanasimba mwezetu, ameifanyia mengi klabu yetu, tunaamini ataendelea mazuri hayo,"amesema.
"Tutaendelea kuisuka timu yetu ili kuendeleza ubora wake. Tuna timu imara. Mimi na Bodi pamoja na menejimenti tunawashukuru sana. Pressure ilikuwa kubwa , lakini tulieni, tupo vizuri sana," amesema Mwenyekiti wa Bodi, Salim Abdallah Muhene (Try Again).

Post a Comment

0 Comments