Kocha Thomas Tuchel asema iwe mvua, iwe jua Chelsea inataka ushindi tu! Leicester City wapewa dozi 3-0 EPL

NA GODFREY NNKO

"Manchester City na Liverpool walifanya hivi kwa miaka na miaka. Wakapeana changamoto na kukimbizana kufikia alama ambazo zilikuwa za kuvutia sana katika miaka iliyopita, na tunapaswa kuthibitisha tuko hivi.
Mambo yalikuwa hivi. (Picha na AFP via Getty Images).

"Haitathibitishwa Jumamosi au wiki ijayo au Krismasi. Ni safari ndefu na tunapaswa kujiimarisha na kujithibitishia kuwa tunaweza kushinda vikwazo na nyakati ngumu. Mambo yanapokuwa magumu, lazima uendelee mbele na kujiimarisha kwa hatua inayofuata. Usisimame. Weka hatua moja baada ya nyingine. Kama kutakuwa na mvua na kuna mechi ngumu huko nje, kuna wapinzani ambao hufanya maisha yetu yasiwe rahisi, lazima tuzipitie kwa kushikamana, na kwa matumaini kwa ajili ya kuiendea njia ya mafanikio,"Kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel ameyabainisha hayo baada ya vijana wake kutoa dozi kwa Leicester City.

Chelsea waliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Ni katika mtanange uliopigwa Novemba 20,2021 katika dimba la King Power.

Mabao ya Chelsea yamefungwa na Antonio Rudiger dakika ya 14, N'Golo Kante dakika ya 28 na Christian Pulisic dakika ya 71.

Matokeo hayo yanaifanya Chelsea inafikisha alama 29 huku kiwa kileleni. Tazama msimamo hapa chini.

Post a Comment

0 Comments