Misingi mitatu ya kuanzishwa TASAF yatajwa

NA JAMES K. MWANAMYOTO

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati ya kuhakikisha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) unatekeleza azma ya kupambana na adui umaskini pamoja na ujinga na maradhi ambao ni kikwazo cha maendeleo ya taifa.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akiwaongoza wajumbe wa kamati yake kujionea bidhaa zinazozalishwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Oldonyowas wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.

Mhe. Chaurembo amesema hayo Novemba 14, 2021 akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kamati yake, iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.

Akizungumzia vita ya TASAF dhidi ya adui ujinga, Mhe. Chaurembo amemuelekeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ndiye mwenye dhamana ya usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za TASAF kuhakikisha wanajenga uzio na mabweni ya wanafunzi wa kiume wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas ili kuimarisha usalama wa wanafunzi hao na kuondokana na tatizo la utoro kwa baadhi ya wanafunzi.

“Pamoja na kazi nzuri ya ujenzi wa madarasa, mabweni ya wanafunzi wa kike na nyumba za Walimu katika shule hii, bado kuna kazi inatakiwa kufanyika, kama tulivyomsikia mwakilishi wa wanafunzi akiomba wajengewe uzio na mabweni ya wanafunzi wa kiume ili wapate mazingira rafiki yatakayowawezesha kupata elimu bora kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla, hivyo kamati yangu inaielekeza Serikali kuzingatia ombi hilo,” Mhe. Chaurembo amesisitiza.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Oldonyowas wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Oldonyowas wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Oldonyowas wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.

Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa alisema, msingi wa utekelezaji wa miradi ya TASAF ni vita dhidi ya adui wa haki ambaye amegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni ujinga, maradhi na umaskini.

Mhe. Mchengerwa amesema ili kupambana na adui ujinga, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametafuta fedha na kuielekeza TASAF kuangalia maeneo ambayo watoto hawapati elimu kwasababu ya kukosa madarasa na mabweni ihakikishe inajenga ili watoto hao waweze kupata elimu itakayowaondolea ujinga.

“Mhe. Diwani amesema, wengi wa watoto wanaosoma shule hii ya Oldonyowas ni watoto wa wafugaji na katika nyakati hizi, wangekuwa wako porini wanasaidia kufuga mifugo ya wazazi wao, lakini leo wako shuleni kwasababu Serikali ya Awamu ya Sita imejenga madarasa na mabweni,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akielezea namna TASAF ilivyowezesha ujenzi wa madarasa, mabweni na nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas iliyoko Kijiji cha Oldonyowas wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakisikiliza ushuhuda wa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas, Everlight Ayo alipokuwa akitoa ushuhuda wa namna walivyonufaika na mradi wa TASAF wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akisisitiza jambo kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Oldonyowas pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.

Mhe. Mchengerwa ameahidi kuwa wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye masomo katika shule hiyo, Serikali itahakikisha inawapatia mikopo kwa asilimia mia moja ili taifa liweze kupata Walimu, Madaktari, Wanasheria na wataalam wengine katika kada mbalimbali wanaotokana na kaya maskini ambao watatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.

Mhe. Mchengerwa amesema adui namba mbili ambaye TASAF inapambana naye ni maradhi ambapo kupitia mradi wa TASAF Awamu ya Nne uliozinduliwa hivi karibuni, Serikali itajenga zahanati katika vijiji vyenye uhitaji ambavyo vinanufaika na mpango huo.

Akizungumzia mapambano yanayofanywa na TASAF dhidi ya adui umaskini, Mhe. Mchengerwa amesema, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kaya zote maskini zinazostahili kuingia kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ziingizwe kwenye mpango huo ili ziweze kuboresha maisha yao.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas, Everlight Ayo akitoa ushuhuda wa namna walivyonufaika na mradi wa TASAF wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiteta jambo na Naibu Waziri wake, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema, utekelezaji wa miradi inayoibuliwa na wananchi itaendelea kwasababu Waziri Mchengerwa ameelekeza kuhakikisha kila sehemu miradi inakoibuliwa wataalam watumike vema kuwasaidia walengwa ili miradi hiyo iwe endelevu na kuwanufaisha.

Kuhusiana na changamoto ya baadhi ya wananchi kulalamika kutoingizwa kwenye mpango, Mhe. Ndejembi amesema, tayari Mhe. Mchengerwa ameshaelekeza Waratibu wa TASAF warejee kwa ajili ya kujiridhisha na kuwaingiza kwenye mpango kwa wale wenye sifa za kunufaika.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga amesema, TASAF itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kulingana na mahitaji yaliyopo na wako tayari kutekeleza maelekezo ya kamati kwa ajili ya kuzinusuru kaya maskini

Post a Comment

0 Comments