Moto wateketeza hoteli za kitalii Zanzibar ikiwemo Villa de Coco ya Jambiani

NA MWANDISHI MAALUM

MOTO ulioanzia jikoni katika Hoteli ya Villa de Coco iliyopo Jambiani jijini Zanzibar umeteketeza hoteli tatu na kuunguza vyumba vingine sita vya hoteli jirani ya nne.

Ni kutokana na upepo mkali wa baharini na zana chache za kuzimia moto usiku wa Novemba 19,2021.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Suleiman Hassan amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema hakuna mtu yeyote aliyedhurika wakiwemo wageni wa hoteli hiyo pamoja na wamiliki wa hoteli.
Kwa miaka kadhaa sasa, matukio ya ajali z moto yamekuwa yakizikabili hoteli mbalimbali za Kitalii jijini Zanzibar.
DIRAMAKINI Blog tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kadri zitakavyotufikia katika chumba chetu cha habari.

Post a Comment

0 Comments