Tanzania yajizatiti kuokoa maelfu ya hekta za misitu inayoteketea kila mwaka

NA HADIJA BAGASHA

AFISA Misitu Mkuu, Emanuel Msofe amesema takwimu zinaonyesha zaidi ya hekta 469,000 za misitu zinapotea kila mwaka na kama hakutakuwa na njia mbalimbali za kudhibiti uharibifu wa misitu inaweza kupelekea vizazi vijavyo vikakosa kufaidi rasilimali hiyo ya misitu.
Msofe ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati wa warsha ya kutambulisha mradi wa FORVAC kwa viongozi wapya walioteuliwa hivi karibuni iliyofanyika jijini Tanga amesema kutokana na changamoto hio kwa sasa zipo njia mbalimbali zinafanyika.

Amesema, njia hizo lazima ziwepo, lakini kutumia huko kuwe kunatokana na mpango ulioandaliwa wa uvunaji wa misitu uwe endelevu ambao kupitia mpango huo msitu ambapo unavunwa eneo dogo la msitu kama asilimia 10 na nyingine linabaki kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu.

Ameongeza pia lazima viwemo vyanzo vya maji na maeneo mbalimbali ambao wanyama wanaishi na kuzaliana.
Afisa Misitu huyo amesema, Idara ya Misitu na Nyuki iliyo chini ya Wizara ya Maliasiali na Utalii inashughulika kuandaa sera, sheria,kanuni na miongozo mbalimbali ya kusimamia misitu kiundelevu hapa Tanzania.

“Kama mliovyoona programu ya Forvac ni matunda ya programu zilizo kwenye mpango wa idara ya misitu na nyuki sasa mnavyojua ni kwamba misitu ipo kwa ajili ya mambo mbalimbali kwanza mifumo ya ikolojia kuhakikisha kuwa kunakuwa na mvua na hewa safi,"amesema.
Amesema, lakini pia kunakuwa na mazingira wezeshi kwa wanyama ambao wanategemea pamoja na binadamu kutokana na kwamba zaidi ya asilimia 90 ya watanzania wanatumia nishati ya kuni mkaa kwa ajili ya kupata huduma ya nishati majumbani.

“Lakini miti mingi zaidi ya asilimia 50 inatoka kwenye misitu maana yake misitu ndio inahifadhi maji sasa changamoto kunakuwa na matumizi ambayo sio endelevu yanachangia kupungua kwa misitu na sasa,"amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mradi wa Forvac.

Awali akizungumza wakati akifungua warsha hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Hashim Mgandilwa alisema wanashukuru na kupongeza Forvac kwa mradi mzuri ambao wanaendelea kuufanya kwao kwa sababu wanakwenda kuvijengea uwezo vijiji ili viweze kuona umuhimu wa kutunza rasilimali misitu.

Amesema pamoja na hayo ni kuongeza mnyororo wa thamani kwa mazao yanayotokana na misitu na kama wanavyojua kadiri dunia inayokwenda wanakumbana na mabadiliko ya tabia ya nchi kana kwamba hali ya hewa haitabiriki baadhi ya viumbe hai navyo nyengine vimekuwa vikipotea.

Naye Meneja wa Mradi wa Forvac kwa upande wa Makao makuu Dodoma, Alex Njahani alisema mradi huo ni wa miaka minne na mwakani mwezi wa saba utafika mwisho kwa hiyo kipindi cha miaka mitatu na zaidi tayari wanachakujivunia kama mradi wamevifanya ambavyo vinaonekana.
Meneja wa Mradi wa Forvac kwa upande wa Makao makuu Dodoma, Alex Njahani.

Amesema, lengo la mradi lilikuwa ni kuongeza thamani mazao ya misitu na tayari kuna kazi zimefanyika na kwa mfano kwenye mkoa wa Tanga wilaya ya Kilindi na Handeni vile vijiji vimeanza kuvuna hivyo tayari mnyororo wa mazao maana yake umeanza.

Meneja huyo alisema pia asali ni mnyororo ambao unajitegemea na wamekwenda hatua nzuri na wilaya ya Handeni tayari wamesaidia mizinga ya nyuki zaidi ya 50 na vifaa vingine vya milioni 98 mwezi Julai mwaka huu na tayari wameanza kuvuna asali tani 1.5 kutokana na mizinga waliowezesha  na hilo wanajivunia kama mradi.

Post a Comment

0 Comments