Prof. Shemdoe: Milioni 210/- kulipa madai ya fedha za mizigo kwa walimu wastaafu jijini Dar es Salaam

NA NTEGHENJWA HOSSEAH

KATIBU Mkuu OR- TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe awaagiza uongozi wa Jiji la Dar es salaam kuanza kuwalipa walimu wa shule za msingi 102 waliostaafu kuanzia mwaka 2018 ambao wanadai fedha za mizigo.
Prof. Shemdoe ametoa agizo hilo Katika Kikao kikichofanyika katika Ukumbi wa Anatoglo jijini Dar es Salaam, Novemba 20,2021 na walimu hao waliostaafu kuanzia mwaka 2015 kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko yao kuhusu mapunjo ya malipo na stahiki zao.

"Suala la kusafirisha mizigo baada ya kustaafu kwa walimu 102 waliostaafu Aprili hadi Disemba, 2018 malipo yao yameshahakikiwa wanadai na Jiji la Dar es Salaam na watalipwa kuanzia wiki ijayo na fedha zilizolipwa ni takribani Shilingi Milioni 210,"amesema.

Na watumishi wengine 102 waliostaafu kati ya Januari hadi Disemba 2019 na 14 waliostaafu mwaka 2021 wenye jumla ya madai ya Shilingi Milioni 368 amemuelekeza Mkurugenzi wa Jiji hilo kufanya ‘realocation’ kwenye Bajeti yake mwezi Desemba ili aweze kuwalipa ifikapo Februari 2022.

Kuhusu madai ya fedha za usumbufu wakati wa kuhamishwa kituo, Prof. Shemdoe amewaelekeza Uongozi wa Jiji kujiridhisha tena kama kweli wengi wao hawastahili kulipwa kwa kuwa walikuwa wanahamishiwa vituo vya kazi ambavyo havikuwagharamu kuhamisha makazi.

Pia mapunjo ya mshahara na areas- Prof. Shemdoe ameahidi kuyafuatilia kwa Katibu Mkuu Utumishi na kuangalia namna bora ya kuyashughulikia.
Kikao kilhudhuriwa na Walimu wastaafu wa shule za Msingi 128 na mtumishi wa Afya mmoja.

Kikao hicho ni utekelezaji wa Agiza la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI alilolitoa Oktoba 28, 2021 wakati Wastaafu hao walipokuja ofisini kwake kuwasilisha changamoto zao.

Post a Comment

0 Comments