Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbili za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Hayo yameelezwa Novemba 29,2021 kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.

"Mosi Mheshimiwa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua ndugu Suleiman Haji Hassan kuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Ardhi.

"Uteuzi wa pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Saleh Mohamed Juma kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali wa Huduma za Matrekta na Zana za Kilimo,"ameeleza Mhandisi Zena kupitia taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo umeanza rasmi Novemba 29, 2021.

Post a Comment

0 Comments