Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi mbalimbali leo Novemba 17,2021

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A. Said uteuzi huo unaanza leo Novemba 17,2021.

Walioteuliwa ni Profesa Moh'd Makame Haji ambaye Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Mwingine ni Dkt.Ali Makame Ussi ambaye ameteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi (SUZA).

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Bibi Kidawa Hamid Saleh kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala ya Serikali wa Uchapaji.

Post a Comment

0 Comments