Rais Samia ashiriki Mkutano wa UWT wa kumpomgeza


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Maisara Zanzibar kwa ajili ya kushiriki katika mkutano ulioandaliwa (UWT) leo tarehe 20 Novemba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Maisara Zanzibar kwa ajili ya kushiriki katika mkutano UWT leo tarehe 20 Novemba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika mkutano wa Jumiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ulioandaliwa na Jumuiya hiyo kwa ajili ya kumpongeza leo tarehe 20 Novemba 2021 katika Viwanja vya Maisara Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,wakati akihutubia katika mkutano wa Jumiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ulioandaliwa na Jumuiya hiyo kwa ajili ya kumpongeza leo tarehe 20 Novemba 2021 katika Viwanja vya Maisara Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya Ngalawa kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Zanzibar kwa niaba ya UWT Mhe. Swahiba Kisasi katika mkutano ulioandaliwa na Jumuiya hiyo kwa ajili ya kumpongeza leo tarehe 20 Novemba 2021 katika Viwanja vya Maisara Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwapongeza na kuwatunza Wasanii wa kikundi cha Tarab cha Culture cha Zanzibar kupitia Msanii Sabina Hassan, kwenye mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika leo tarehe 20 Novemba 2021 katika Viwanja vya Maisara Zanzibar.(PICHA NA IKULU).

Post a Comment

0 Comments