Hoteli za Spice Island,Fun Beach,Cobe na Villa de Coco zateketea kwa moto jijini Zanzibar


NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MATUKIO ya ajali za moto nchini yameendelea kuwa kikwanzo ambapo katika tukio la kusikitisha, hoteli nne za kitalii zimeteketea kwa moto huku wageni na wafanyakazi wa hoteli hizo wakinusurika kifo jijini Zanzibar.
Tukio hilo la Novemba 19, 2021 limetokea maeneo ya Jambiani katika Mkoa wa Kusini Unguja huku chanzo na hasara vikiwa bado havijajulikana hadi sasa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Suleiman Hassan amesema hoteli tatu kati ya hizo zimeteketea kabisa na hakuna kitu ambacho kimeokolewa isipokuwa wageni waliokuwa ndani ya hoteli hizo.
Amesema, hakuna mgeni au mfanyakazi aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa kutokana na moto huo uliotajwa kuwa mkubwa kutokana na paa za hoteli hizo kuwa za makundi.

“Moto huo ulianza kuteketeza Hoteli ya Villa de Coco na kisha ukasambaa katika hoteli zengine ambazo zipo karibu na hoteli hiyo,” amesema.
Hoteli nyingine ni Spice Island ambayo imeungua vyumba sita vya kulala wageni, Fun Beach na Cobe ambazo zimeteketea zote na wageni wake waliharakishwa kutolewa na kuhifadhiwa katika hoteli zingine.

Kamanda Hassan amesema chanzo chake bado hakijajulikana, lakini taarifa za awali inadaiwa kuwa ni hitilafu za jiko katika hoteli ya Villa de Coco.

Aidha, kwa mujibu wa Kamanda huyo, hoteli hizo zinamilikiwa na wamiliki tofauti ambao ni rai wa kigeni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news