NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mheshimiwa David Kafulila leo Novemba 10,2021 amemwelekeza Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Simiyu, Joshua Msuya kukagua malipo yote ya AMCOS.
Ameyasema hayo wakati akihutubia Baraza la Madiwani Wilaya ya Maswa mkoani hapa huku akisisitiza kuwa, hatua za haraka zitachukuliwa ili kumneemesha mkulima na si kumdidimiza.
Pia Kafulila amewataka wakulima wote wa Pamba kujiunga na ushirika kwani atahakikisha kuwa anaondoa virusi wote kuanzia maofisa ushirika halmashauri mpaka viongozi wa AMCOS.
"Lengo ni kuhakikisha Serikali kwa kushirikia na ushirika tunamkomboa mkulima mdogo, na hilo lengo litafikiwa kama ilivyokuwa miongo kadhaa baada ya Uhuru,"amesema RC Kafulila.