RC Kafulila amsimamisha kazi Afisa Ushirika kwa tuhuma za kuvujisha Milioni 63/-

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa David Kafulila ameagiza kusimamishwa kazi kwa Afisa Ushirika Wilaya ya Maswa, Bw. Daud Makoye kwa tuhuma za ubadhirifu wa shilingi milioni 62 zinazohusisha AMCOS 17.

Ni baada ya kubaini kwamba ufisadi huo ulihusisha Afisa ushirika huyo na kuelekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inakamilisha uchunguzi haraka na kumfikisha mahakamani.

Mhe. Kafulila amechukua hatua hiyo kutokana na taarifa za awali kuonesha kwamba viongozi wa AMCOS Maswa walikuwa wanatoa pesa benki na kumkabidhi afisa Ushirika huyo Bw. Makoye ili akalipe kwa mamlaka zingine kama Bodi ya Pamba, Tume ya Ushirika na SIMCU.
RC Kafulila ametoa uamuzi huo leo Novemba 10, 2021 wakati anahutubia Baraza la Madiwani Wilaya ya Maswa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news