RC Kunenge ajitoa kwa nguvu zote kukomesha migogoro ya ardhi

NA ROTARY HAULE

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amelazimika kuchukua hatua ya kuwakutanisha wadau mbalimbali wa ardhi wakiwemo wakulima na wafugaji kwa ajili ya kujadili namna ya kupata njia sahihi zitakazosaidia kukomesha migogoro inayotokana na ardhi.
Kunenge ameitisha kikao hicho Novemba 16,2021 katika ofisi yake iliyopo Mjini Kibaha ambapo miongoni wa wadau walioshiriki mkutano huo ni pamoja na wakulima na wafugaji,taasisi zinazojihusisha na ardhi,wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wadau wengine.

Katika kikao hicho Kunenge aliwaeleza wadau hao kuwa amechoshwa na migogoro ya ardhi inayotokea mara kwa mara mkoani kwake huku akisema kikao hicho ameitisha ili kupata njia sahihi ya kukomesha migogoro hiyo.

Amesema kuwa,jambo pekee linalompa changamoto ni suala la migogoro ya ardhi ambapo alisema kwa sasa lazima ifike mwisho na majibu ya utatuzi wa jambo hilo yapatikane.

Alisema kuwa, haiwezekani kuona kila siku inazuka migogoro ambayo inaathiri hali za wananchi kwa kusababisha mapigano yanayoleta vifo,watu kujeruhiwa na wengine kukwamisha kiuchumi halafu viongozi wakalichekea.

"Mimi nataka migogoro ya ardhi Pwani hiwe historia na nitafanyakazi bila kumuogopa mtu ,kwahiyo lazima wakulima ,wafugaji na sisi wote tuliokuwa humu tutoe michango yetu ambayo itasaidia kumaliza migogoro ya ardhi,"alisema Kunenge.

Kunenge,amesema watu wanapoteza maisha kwa kuchomana visu,kukatana mapanga,kupigana mikuki halafu viongozi hawajali kwahiyo haiwezekani kuchekea mambo ambayo yanahatarisha wananchi.


"Leo nataka wote mtoe solution (suluhusho) ya migogoro ya ardhi na kama wewe umekuja hapa kunisikiliza mimi na hauna solution yoyote ni bora uondoke maana utakuwa hujasaidia kitu,"amesema Kunenge.

Kunenge ,ameongeza kuwa kama kuna mambo ambayo hatuwezi kubembelezana ni hili na sababu wananchi wanapoteza maisha kwa mambo hayo,uchumi unashuka kwahiyo umefika wakati wa kupambana nalo.

Alisema kuwa,wale wore ambao wamesababisha migogoro hiyo watafutwe na ikiwezekana kama wapo na wao waondoke maana ndio walisababisha kufika hapa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Chama cha Wafugaji inayoshughulikia migogoro ya ardhi, George Kifuko,alisema jambo lililofikiwa na mkuu wa mkoa ni zuri na litasaidia kupunguza migogoro hiyo.

Hata hivyo,alisema jambo kubwa litakalosaidia kupunguza migogoro hiyo ni pamoja na kuweka mipango bora ya matumizi ya ardhi kwa kuhakikisha wafugaji wanatengewa maeneo yao bila kuingiliana na wakulima.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Abdallah akizungumza katika kikao cha wadau wa ardhi kilichofanyika Kibaha Mjini. (Picha na Rotary Haule).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news