Tanzanite yaichapa Burundi 3-2 michuano ya CECAFA

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Wanawake wameendelea kuonyesha ushujaa katika soka la Kimataifa baada ya kuendelea kuitoa kimasomaso Tanzania katika anga la Kimataifa.
Ni baada ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 (timu ya Tanzanite) kuichapa Burundi 3-2 leo Uwanja wa FTC Njeru nchini Uganda kupitia michuano ya CECAFA.

Mabao ya Tanzanite leo yamefungwa na Mwamvua Haruna dakika ya 60 kwa penalti, Clara Luvanga dakika ya 80 na Emiliana Isaya dakika ya 83.

Aidha, Tanzanite iliyoshinda 1-0 dhidi ya Eritrea Jumamosi iliyopita bao pekee la Clara Luvanga dakika ya 90 itashuka tena dimbani Jumatano kumenyana na Ethiopia, kabla ya kuivaa Uganda Jumamosi na kukamilisha mechi zake kwa kucheza na Djibouti Novemba 9, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments