Vyama 11 vyalitaka Jimbo la Ngorogoro, vitatu vyajiweka kando

NA MWANDISHI MAALUM

Wagombea wa vyama Kumi na Moja katika jimbo la Ngorongoro lilipo mkoani Arusha wameteuliwa na Tume ya Taifa ya uchaguizi(NEC) kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro,Dkt.Jumaa Mhina .

Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Dkt.Jumaa Mhina amesema,awali vyama 14 vilichukua fomu ya kuwania nafasi hiyo lakini mpaka zoezi hilo linafungwa leo Novemba 15 saa 10:00 ni wagombea wa vyama 11 pekee ndiyo waliokuwa wamerudisha fomu zao.

Ametaja wagombea hao kuwa ni pamoja na Emmanuel Shangai (CCM),Simon Bayo (SAU), Amina Mcheka (NLD), Mary Daudi (UPDP), Frida Nnko (UMD),Paulo Makuru (UDP),Shafii Kitundu (ADC), Feruziy Feruziyson (NRA),Simon Ngilisho (DEMOKRASIA MAKINI), Jonson Gagu (ACT WAZALENDO) na Zuberi Hamis (ADA TADEA).

Ametaja wagombea ambao hawakurudisha fomu ni pamoja na Singa Klekwa (CCK), Mgina Mustafa (AFD ) na Donald Laizer (TLP).

"Kwa mujibu wa ratiba ya NEC kampeni za wagombea wote zitaanza Novemba 16 mwaka huu hadi Disemba 10 mwaka huu hivyo ninaomba vyama vyote viwasilishe ratiba zao ili tuweze kuwapangia ratiba nzuri ambayo wagombea hawakutana kwenye kata moja haswa katika siku za kuzindua kampeni. Tunataka kila mgombea afanye kampeni kwa huru bila kuingiliana,"amesema.

Dkt.Mhina amewataka wagombea hao kufanya kampeni za kistaarabu kwa kila mgombea kunadi sera za chama chake badala ya kufanya kampeni za kupakana matope.

“Wakati wote wa kampeni naomba mtumie lugha za staha ,heshima ambazo hazidhalilishi mgombea mwingime.Shindaneni kwa sera za vyama vyenu ili kuepuka kampeni za kupakana matope,"amesema.

Amesema, tume itatenda haki kwa vyama vyote ikiwa ni pamoja na kamati ya maadili ambayo itashughulikia malalamiko yote yatakayowasishwa na vyama au wagombea wanaogombea ubunge katika jimbo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news