Wafanyabiashara wa nyama Oman waona fursa Tanzania, kuitumia Bandari ya Tanga

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WAFANYABIASHARA maarufu nchini Oman wanatarajiwa kufanya ziara nchini Tanzania kuanzia Novemba 25, 2021 kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kupata eneo mkoani Tanga la kukusanyia mifugo hai ya kusafirisha Oman kupitia Bandari ya Tanga.
Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima akipokea zawadi kutoka kwa Bw. Mohamed S. Aldarai, kiongozi wa ujumbe wa wafanyabiashara ya nyama nchini Oman. Kushoto ni Bw. Tahir Bakar Khamis ambaye ni Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania Oman.

Wafanyabiashara hao ambao ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Abu Suleiman Al-Darai Trading &Services, Bw. Mohamed S. Aldarai; Afisa Mtendaji Mkuu wa Desert Cold Store LLC, Dkt. Munawar H. Pardhan; Mkurugenzi wa Desert Cold Store LLC, Bw. Aasim M. Pardhan na Mkurugenzi wa IKTIMAl Trading Company LLC, Bw. Salem Al Dighaishi awali walikuwa wanasafirisha nyama iliyogandishwa tani 240 kwa mwezi kutoka nchini walifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima hivi karibuni kuhusu taratibu za utekelezaji wa biashara yao hiyo.

Mhe. Balozi aliwapongeza wafanyabiashara hao kwa kuonesha nia ya kufanya biashara na Tanzania kwani itasaidia kubadilisha urari wa biashara kati ya nchi hizi mbili ambao kwa sasa inaonesha Oman inauza zaidi nchini Tanzania.

Aliwaahidi wafanyabiashara hao kuwa atawakutanisha na Mamlaka husika nchini Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Edwin Rutageruka ili kukamilisha taratibu husika.
Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabishara wa nyama. Kutoka kulia ni Bw. Salem Al Dighaishi – Mkurugenzi wa IKTIMAl Trading Company LLC; Bw. Mohamed S. Aldarai – Mkurugenzi Mwendeshaji wa Abu Suleiman Al-Darai Trading &Services; Dkt. Munawar H. Pardhan – Afisa Mtendaji Mkuu wa Desert Cold Store LLC; na Bw. Aasim M. Pardhan – Mkurugenzi wa Desert Cold Store LLC.

Wafanyabiashara hao walielezea malengo yao ya baadaye ni kufanyabiashara ya kusafirisha matunda kutoka nchini kwenda Oman na nchi nyingine za ghuba, jambo ambalo litasaidia wakulima wa Tanzania kupata soko na kuondoa uharibifu wa matunda yanayoharibika kwa kukosa soko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news