Wanafunzi 907,802 wapangiwa kwenda Kidato cha Kwanza 2022

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SERIKALI imetangaza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022 huku ikisema imawapa kipambele wanafunzi wa vijijini shule za kitaifa za bweni.
Akitangaza uchaguzi huo leo Jumatano Novemba 24, 2021, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Ummy Mwalimu amesema nafasi zinazokwenda kwa wanafunzi wa bweni ni za shule za kitaifa.

Katika upangaji wa mwaka huu wanafunzi wote 907,802 waliofaulu mtihani wamepangiwa kuanza masomo Januari 17, 2022 kwa wakati mmoja baada ya maandalizi ya Serikali.

Upangaji huo hautahusisha wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi ambao wao watapangiwa kulingana na alama zao na kwa mwaka 2022 wanafunzi waliofaulu zaidi na kupangiwa ni wanafunzi 4188.

"Wanafunzi waliopangiwa shule za bweni za Kitaifa ni 1989 na hapa tumechukua zaidi wanafunzi wa vijijini lakini kwenye majiji na halmashauri tumeangalia sana wenye uhitaji tu," amesema Mwalimu.Bofya hapa kuona majina>>>

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

SELECTION FORM ONE - 2022

Au bonyeza mkoa wako chini



ARUSHA

DAR ES SALAAM

DODOMA

IRINGA

KAGERA

KIGOMA

KILIMANJARO

LINDI

MARA

MBEYA

MOROGORO

MTWARA

MWANZA

PWANI

RUKWA

RUVUMA

SHINYANGA

SINGIDA

TABORA

TANGA

MANYARA

GEITA

KATAVI

NJOMBE

SIMIYU

SONGWE


Waziri ametoa sababu za kupangiwa zaidi kwa wanafunzi wa vijijini katika shule za bweni za Kitaifa kwamba kunatokana na uamuzi wa Serikali wa kujali wanafunzi wote wapate elimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news