Wanawake waishukuru Manyara Press Club kwa elimu bora ya afya

NA MARY MARGWE

Wanawake na wasichana wa Kata ya Endasaki wilayani Hanang' mkoani Manyara wameishukuru Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Manyara (MNRPC) kwa kuwapatia elimu juu ya haki ya afya ya uzazi salama, kupitia mradi ambao kwao ni mpya na mkubwa wenye kubeba maisha yao.

Baadhi ya wanawake na wasichana wa Kata ya Endasaki wilayani Hanang' mkoani Manyara wakiwa kwenye mafunzo ya siku moja juu ya haki ya afya ya uzazi salama, yaliyowezeshwa na Klabu ya Waaandishi wa Habari mkoani Manyara (MNRPC) chini ya ufadhili wa Women Fund Trust (WFT). (NA MARY MARGWE).

Mafunzo hayo yaliyotolewa na Manyara Press Club (MPC ) chini ya ufadhili wa Women Fund Trust ( WFT ) ambapo walitoa shilingi milioni 10 kwa klabu hiyo ili kutekeleza mradi huo wa miezi sita katika wilaya ya Hanang' na Babati.

Wakiongea kwa nyakati tofauti na DIRAMAKINI BLOG mmoja wa akina mama hao aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth January amesema ikizungumziwa tu afya ya uzazi moja kwa moja utakuwa umegusa maisha ya mwanamke hivyo ijulikane kuwa afya bora ndio msingi mkuu wa maisha. hivyo elimu waliyoipata kwao ni nguzo thabiti ya afya salama ya uzazi.

"Binafsi kabisa nichukue fursa hii kuishukuru Manyara Press Club kwa kuliona hii kuwa ni tatizo kwa kundi la wanawake na wasichana na hatimaye kutuletea elimu hii ambayo kwetu ni msaada na mkombozi mkubwa kwa afya zetu na wasichana wetu, kwani kupitia mafunzo haya tutakukuwa tumepata elimu kubwa ya kutufumbua macho katika masuala ya haki ya afya ya uzazi,"amesema January.

January amesema, wengi walikuwa wakiangaika na njia salama ya uzazi wa mpango, kumbe mtaalamu amewaambia njia zote ni salama ndio maana zimeletwa kwao wazitumie, isipokuwa iwapo zinawaletea shida wametakiwa kurudi hospitali ili kuangalia ni njia ipi inayomfaa zaidi.

Naye Salome Athanas aliilalamikia njia ya uzazi wa mpango kuwa si nzuri, kwani zinafanya akose kabisa kuona mzunguko wake wa damu ya kila mwezi.

Mnufaika mwingine wa mafunzo hayo, Amina Michael amesema njia hizo zimemsababishia mguu wake kuvimba huku mishipa ikiwa imesimama na kumsababishia maumivu makali sana.

Akijibu hoja hizo Afisa Afya wa Wilaya ya Hanang' mkoani humo, Anasia Mariki amesema njia zote za uzazi wa mpango ni nzuri na salama, isipokua huwa zina vichocheo na maudhi madogo madogo, inategemea na mwili wa mtu.

Amesema zingekuwa na madhara zisingeletwa nchini wananchi waumie, ni njia nzuri, bora na salama ndio maana zimeletwa kwa lengo la kutumika, hivyo iwapo kuna utofauti yoyote kinachotakiwa ni kwenda hospitalini kupata ushauri kutoka kwa watoa huduma ili kupata njia itakayoendana naye.

"Ndugu washiriki naomba muelewe kuwa malalamiko yenu yote nimeyasikia na nimeyaelewa isipokua tambueni kuwa njia zote za uzazi wa mpango ni nzuri na salama, na hayo madhara mliyoyasema ni sawa na mtu anayekunywa dawa ya kwinini wengine huwa zinawadhuru masikio huwa hayasikii, lakini wengine huwa zinawafaa, ndivyo na hizo njia zilivyo,lakini niwatoe hofu kuwa njia zote ni nzuri na salama,"amesema Anasia Mariki.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa MNRPC, Zacharia Mtigandi,klabu hiyo imefanikiwa kupata mradi wenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Women Fund Trust (WFT).

Mtigandi amesema, mradi huo utahusisha wanawake na wasichana wa wilaya ya Hanang' na Babati kuchukua hatua juu ya haki ya afya ya uzazi kwa makundi hayo.

"Mradi huu utakua wa miezi sita, unaendelea kutekelezwa kwa kata za Endasaki wilayani Hanang' na Kata ya Sigino na Riroda kwa Wilaya ya Babati mkoani Manyara,"amesema Mwenyekiti wa Manyara Press Cub, Zacharia Mtigandi.

Baadhi ya wanawake na wasichana wa Kata ya Endasaki wilayani Hanang' mkoani Manyara wakiwa kwenye mafunzo ya siku moja juu ya haki ya afya ya uzazi salama, yaliyowezeshwa na Klabu ya Waaandishi wa Habari mkoani Manyara (MNRPC) chini ya ufadhili wa Women Fund Trust (WFT). (NA MARY MARGWE).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news