Waziri Ummy ateua Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo

NA GODFREY NNKO

KUFUATIA uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumteua Prof. Joseph Kuzilwa, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Ummy Mwalimu kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Chuo cha Serikali za Mitaa Sura ya 396 iliyorejewa mwaka 2002 amefanya uteuzi wa wajumbe wa bodi ya chuo hicho.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah ambapo walioteuliwa ni wajumbe mbalimbali.

Miongoni mwa wajumbe hao ni Prof.Honest Prosper Ngowi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Bw.Richard Thomas Mfugale ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa. Unaweza kusoma, Maamuzi ya Serikali kuhusu ukusanyaji ushuru wa maegesho.

Wengine ni Bi.Josephine Rwehumbiza ambaye ni Mhadhiri Msaidizi, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dkt.Provident Dimoso ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Bw. Elisante M. Mbwilo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Uendelezaji Rasilimali Watu, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mbali na hao wengine ni Bw.Nuru R.Namoroma ambaye ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Serikali za Mitaaa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw.Mohamed Ahmed Maje ambaye ni Afisa Elimu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Bw.Januari Alex Daudi ambaye ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Novemba 5, 2021, bodi hiyo ya Chuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo itaongoza kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe ya uteuzi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Ummy Mwalimu. (NA MAKTABA).

Post a Comment

0 Comments