Waziri Ummy atoa maagizo kuhusu ujenzi wa zahanati

NA ANGELA MSIMBIRA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Saidi Mtanda kuunda kamati ndogo ya uchunguzi matumizi ya shilingi milioni 50 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati ya Chemka,Halmashauri ya Wilaya Hai mkoani Kilimanjaro.
Akikagua ujenzi wa zahanati hiyo Novemba 16, 2021 katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Waziri Ummy amesema hajaridhishwa na matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa zahanati hiyo iliyoanza kujengwa tangu mwaka 2016 lakini hadi sasa bado ujenzi haujakamilika.

“Haiwezekani Serikali ikatoa fedha kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati hiyo, lakini bado haijakamilika huku wananchi wakilalmika kujitoa kwa nguvu zote kuhakikisha Zahanati hiyo inakamilika kwa wakati, lakini mpaka sasa haijakamilika, hili siwezi kulivumilia, hivyo nakuagiza Mkuu Wilaya huyo kuchunguza matumizi ya fedha hizo fedha hizo,"amesema Waziri Ummy.

Ameendelea kufafanua kuwa kiasi cha shilingi milioni 25 zilitolewa na halmashauri ya Wilaya ya Hai, kupitia mapato ya ndani, wananchi walichangia kiasi cha shilingi milioni 48 huku serikali kuu ikitoa kiasi cha shilingi milioni 50, lakini bado ujenzi huo haujakamilika jambo ambalo linawakosesha wananchi haki ya kupata huduma bora za afya na kupata huduma hiyo karibu na maeneo yao.

Waziri Ummy amesema, mara baada ya kupatiwa taarifa kamili ya matumizi ya fedha hizo iwapo itagundulika kutumika kinyume na utaratibu hata sita kuwachukulia hatua wahusika wote watakaodhibitishwa kutumia fedha hizo kinyume na utaratibu.

Aidha, Mradi wa Ujenzi wa Zahanati ya Chemka ulianza mwaka 2016 kwa nguvu za wananchi, na ulilenga kutatua kero ya upatikanaji wa huduma bora za afya ambapo kiasi cha shilingi milioni 120 zimetumika ujenzi wa zahanati hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news