Wazo waja na programu unganishi ya walinzi binafsi kudhibiti uhalifu

NA RACHEL BALAMA

KATA ya Wazo imejipanga kukabiliana na vitendo vya uhalifu kupitia programu unganishi ya walinzi binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea Makamanda,Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambae pia ni Mtendaji wa Kata ya Wazo, Husna Nondo amesema kuna maeneo ambayo yamekua yakifanywa ni sehemu ya machimbo ya uhalifu inayopelekea kuzalishwa kwa vibaka,waporaji na wezi wa mifugo.

"Ni kata kubwa mno, hivyo utaona hata mkusanyiko wa watu ni mkubwa. Lakini kutokana na kuwepo uhalifu inapelekea hata watu kushindwa kufanya maendeleo kwa kuhofia usalama wao na mali zao hasa maeneo ya Kilimahewa juu na Kata ya Wazo yenyewe."

Hata hivyo Nondo amewapongeza programu unganishi ya walinzi binafsi nchini (TPSIST) kwa kuona ipo haja ya kutoa ulinzi shirikishi na elimishi kwa kata ya Wazo ili kusaidia kuboresha usalama wa raia na mali zao.

"Kupitia muunganiko huu tunategemea kukomesha na kutokomeza uhalifu katika Kata zetu ili kuweza kufanya maendeleo na kuona kata zetu ni sehemu ya uwekezaji."

Kwa upande wake Mkurugenzi wa program unganishi ya Walinzi binafsi nchini (TPSIS), David Rwegoshola amesema ni vyema jamii ikatoa elimu shirikishi kwa vijana ambao tayari wameshajiingiza kwenye vitendo viovu ili kuangalia kwa jinsi gani wataweza kubadili taswira za vijana hao kuwa Maisha ya uhalifu ni ya utajiri.

"Vijana wengi hasa wahalifu wanaamini kuwa ukijiingiza kwenye vitendo viovu ndio umetoboa Maisha au kufanikiwa lakini Hali hii ikiweza kudhibitiwa na jamii kuonyesha jitihada za kutoa Elimu shirikishi tunaweza kutokomeza kabisa vitendo vya uhalifu wa kila aina,"amesema.

Pia ameeleza kwa namna gani sskari hao 90 ambao wamehaidi kuboresha usalama katika Kata ya Kilimahewa juu na kata ya Wazo na kupitia programu unganishi wataweza kupambana na vijana walioshindikana.

"Ni askari ambao wataboresha ulinzi na usalama katika Kata hii na tunategemea kazi itafanyika ya kusafisha na kupewa Ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wananchi wenyewe na kutoa taarifa sehemu zenye magenge ya vibaka,Wala unga,Majambazi na Wale wanaojiita vishandu."

Nae Mwenyekiti wa wenyeviti katika Kata ya Wazo, Medard Mashauri ameongeza kuwa Kutokana na ukubwa wa Kata ya Wazo hata watu nao wamekuwa wengi na kupelekea wageni kuingia katika Makazi na kufanya uhalifu.

"Raia wa kigeni hasa kabila la Wanyasa kutoka nchi ya Malawi wamekua wakijihusisha na uhalifu wa kuvunja maduka kwa kutumia tindikali,Kata ya Wazo ina wakazi wengi na miongoni mwao wanapata posho kupitia raia hao wa kigeni na kutunza siri sawa na kuwapatia uhakika wa kuishi sehemu hiyo,"amesema.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ujio wa Makamanda hao utakua chachu ya kuimarisha ulinzi na kuhakikisha wanatoa Elimu kwa kuwapa vijana muongozo jinsi ya kutafuta kipato cha halali pasipo kujiingizia kwenye vitendo vya uhalifu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news